MOHAMED HAMAD
Serikali wilayani Kiteto mkoani Manyara imesema, takwimu zinazotumika
katika mipango mbalimbali ya maendeleo zikiwemo idadi ya watu na
makazi, ukubwa wa eneo, pamoja na idadi ya mifugo sio sahihi, kutokana
na zoezi kuanza la kubainishwa upya mipaka ya vijiji na wilaya
Hayo yameelezwa na Nockodemus John katibu Tawala wa wilaya ya Kiteto
wakati akionyesha changamoto zinazowakabili viongozi wa Serikali na
jinsi wanavyokabiliana nazo kutokana na migogoro ya ardhi
inayoikabili wilaya hiyo
“Viongozi wa Serikali hatuna kazi zingine za maendeleo tunazofanya
kama walivyo Viongozi wa maeneio mengine badala yake kila siku, mwezi
na mwaka tumekuwa tukishuhulikia migogoro ya ardhi kati ya wakulima na
wafugaji”alisema Katibu Tawala huyo
Serikali imejipanga kufanya sensa ya idadi ya watu na makazi, mifugo,
idadi ya mashamba ya wakulima na ukubwa wake na kuandaa mpango wa
matumizi bora ya ardhi kuepuka migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo
hujitokeza kila mara alisema
Kila mara migogoro ya wakulima na wafugaji imekuwa ikijitokeza na hata
vijiji na wilaya jambo lililosukuma uongozi wa Taifa kuingilia kati
kuamua kupima eneo lote la wilaya ya Kiteto ili kuanza upya mpango na
kuusimamia vizuri kuepuka migogoro hiyo
Alisema takwimu zinazotumika za idadi ya watu na makazi, idadi ya
mifugo, ukubwa wa eneo la Kiteto, pamoja na eneo la wakulima na
wafugaji sio sahihi na zimekuwa zikitumika katika kmipango mablimbali
ya Serikali akisema hazina uhalisia
Zoezi la upimaji ardhi halikukamilika na wapima waliondoka kutokana na
sababu mbalimbali zikiwemo ukwasi wa fedha wakati huo hivyo kufanya
wananchi hao kuwa njia panda wasijue chakufanya huku imani kubwa
ikielezwa kukamilika kwa zoezi hulo ndio kutakuwa mwarubaini wa
migogoro Kiteto
Katika hatua hiyo alisema viongozi wa wilaya ya Kiteto ngazi
mbalimbali hawafahamu idadi ya mifugo, ukubwa maeneo na kuiomba
Serikali ngazi ya Taifa kuharakisha hatua mbili zilizobakia kati ya
ahtua zilizofanyika katika zoezi zima la upimaji wa ardhi Kiteto
Kwa upande wake Bakari Maunganya (mwananchi) alisema kukosekana kwa
taarifa sahihi kwa wakati kunachangia kutopata maendeleo ya eneo
husika na kuiomba Serikali iharakishe mpango huo ambao ndio tumaini la
wana-Kiteto
Naye Meshaki Saskar (mfugaji) alisema pamoja na kuwa na mpango huo
viongozi wana nafasi kubwa kuutekeleza kwani hata sasa wakitaka
matatizo hayawezi kujitokeza na kuongeza kuwa tatizo liko katika dhana
ya uwajibikaji kwa viongozi
Maoni
Chapisha Maoni