Mkuu wa wilaya ya Kiteto Kanali Samuel Nzoka akichangia jambo kwenye kikao cha wadau wa elimu Kiteto Picha na Mohamed Hamad
Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Kiteto Bosco Ndunguru akichangia jambo kikao cha wadau wa elimu jana
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Lairumbe Mollel akichangia jambo kwenye kikao cha wadau wa elimu Kiteto
Afisa elimu Sekondari Rajabu Chongoe akitoa taarifa ya hali ya elimu Kiteto
Afisa mkurugenzi wa udhibiti wa ubora wa shule Fidelis Kyarwenda akifafanua jambo
Kaimu Afisa elimu shule za msingi Omar Mlekwa akitoa taarifa ya hali ya elimu Kiteto kwa wadau
Mdau wa elimu kutoka hifadhi ya WMA Kiteto akichangia jambo
DED na DAS Kiteto wakisikiliza jambo kwa makini kikao cha wadau wa elimu
wenyekiti wa SULEDO Sharifu Lemanda kwenye kikao cha wadau wa elimu Kiteto
Uongozi wa wilaya ya Kiteto kushoto DED Bosco Ndunguru, anayefuata DAS Necodemus John, anayefuata DC Kanal Samuel Nzoka anayefuata Makamu mwenyekiti wa Halmashauri Yahaya masumbuko Picha na Mohamed Hamad Kiteto
Wanafunzi wa sekondari ya kibaya wilayani Kiteto hapo juu wakiwa kwenye jengo la maabara ambalo halijakamilika baada ya kukosa darasa huku wakiwa wamekaa chini kwa kukosa madawati picha na Mohamed Hamad
Wadau wa elimu wilayani Kiteto wakiwa katika kikao kujadili changamoto zinazokabili sekta ya elimu wilayani humo Picha na Mohamed Hamad
Shule ya Sekondari Kibaya hapo chini iliyoanzishwa miaka minne iliyopita inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa,nyumba za walimu,viti na meza, hali inayosababisha adha kwa wanafunzi katika masomo Picha na Mohamed Hamad
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Kibaya wilayani Kiteto wakionyesha tofali wanazotumia kukalia baada ya kukosa viti na meza pamoja na darasa Picha na Mohamed Hamad Kiteto
NA.MOHAMED HAMAD
Serikali wilayani Kiteto
mkoani Manyara imesema itahakikisha inamaliza tatizo la wanafunzi kukaa chini
kwa kutengeneza madawati yanayotokana na msitu wa mbao wa SULEDO uliopo wilayani humo
Akizungumza mbele ya kikao
cha wadau wa elimu kilichofanyika march 10 mwaka huu, mkurugenzi mtendaji wa
Halmashauri ya wilaya Bosco Ndunguru alisema alisema, Serikali imelazimika
kutumia msitu wa SULEDO kukabiliana na
tatizo hilo
“Wakati mwingine watu
wanaweza kukushangaa kiongozi wa eneo husika juu ya tatizo la wanafunzi kukaa chini wakati
tuna misitu kama ule wa SULEDO ambao
unanufaisha maeneo mengine kwa suala la mbao”alisema Mkurugenzi huyo
Wakichangia uboreshaji wa
sekta ya elimu Hassani Konki,Ramadhani Machaku,Ibrahimu Msindo wadau wa elimu
wilayani humo walisema ili kuimarisha sekta hiyo viongozi wa Serikali hawana
budi kutimiza wajibu wao
“Kiongozi wa Serikali tumempa
mamlaka kusiomamia sheria zilizopo ikiwemo ya elimu, sasa kama
wanashindwa na kubaki kulalamika kwa kutoa kisingizio cha wananchi hawana
uelewa mzuri juu ya suala la elimu watatuchelewesha”
“Tunataka kusikia Serikali
wilayani Kiteto ikitoa matamko mazito na hata kuchukua hatua dhidi ya watu
wanaovunja sheria ili mwisho wa siku tuone elimu ikiimarika kwa wanafunzi
kupata elimu”alisema Ibrahimu Msindo
Kwa upande wake Hassani Konki
mdau wa elimu alisema, ili sekta ya elimu iweze kuimarika waalimu wanapaswa
kupatiwa haki zao pamoja na kupunguza uhaba wa waalimu shuleni kwa kuajiriwa
wengine akisisitiza haki huendana na wajibu
Mkuu wa wilaya ya Kiteto
Kanal Samuel Nzoka aliwataka wadau wa elimu kuona kuwa kuna wajibu wa kuchangia
sekta hiyo kwa hali na mali
kuwa elimu bure iliyosemwa na serikali haina maana ya mzazi hawezi kuchangia
Kwa upande wake kaimu afisa
elimu shule za msingi Omari Mlekwa alisema wilaya inaupungufu wa madawati 7,777
kati ya 7,160 yaliyopo kutokana na uchangiaji hafifu wa wazazi kabla ya elimu
bure
Afisa elimu sekondari Rajabu
Chongowe akiwasilisha taarifa ya elimu kwa wadau hao alisema jumla ya viti 1478
na meza 1710 zinahitajika kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2016 ili
waweze kusoma wakiwa wamekaa tofauti na ilivyo sasa wengi wao kukaa chini
‘Mhesimiwa mwenyekiti mkakati
uliopo ni kwamba, tumeweza kuzungumza na uongozi wa hifadhi ya msitu wa SULEDO
na kukubaliana nao kuwa watatengeneza madawati kwa bei ya kutusaidia ili
kuondoa adha kwa wanafunzi hawa
Mwenyekiti wa Halmashauri ya
wilaya Lairumbe Mollel aliwashukuru wadau hao wakiwemo uongozi wa msiti wa
SULEDO kwa kukubali kutengeneza madawati kwa bei ya chini, pamoja na uongozi wa
umoja wa vijiji vilivyounga hifadhi ya wanyama WMA kwa kusaidia sekta ya elimu
madawati pamoja na vyumba vya madarasa
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni