Wanafunzi 120 Sekondari ya Kibaya Kiteto hawana madarasa,madawati

























NA.MOHAMED HAMAD
Zaidi ya wanafuzi 120 wa shule ya shule sekondari Kibaya iliyopo Kiteto mkoani Manyara iliyoanzishwa mwaka 2013, wanalazimika kukalia kanga na mifuko aina ya salfeti kutokana na kukosa viti na meza darasani

Wanafunzi hao ni kidato cha kwanza ambao waliripoti shuleni na kukosa vyumba vya madarasa, viti na meza hali iliyowalazimu waalimu wao kuwaagiza kanga na mifuko ya kukalia huku wakiwa kwenye majengo mawili ya maabara kama madarasa ambayo hayajakamilika

Akizungumza na MTANZANIA kwa masharti ya kutotajwa majina yake shuleni hapo mmoja wa waalimu hao alisema, shule hiyo ilianzishwa mwaka 2013 kwa msukumo wa sera ya kila kata kuwa na sekondari jambo ambalo imeonekana wazazi hawakujiandaa kuihudumia

Kwa mujibu wa mwalimu huyo alisema shule  ina madarasa 5 ambapo darasa 1 linatumiwa na kidato cha 3, madarasa 2 yanatumiwa na kidato cha 4 wa masomo ya Sayansi na Arts, madarasa 2 kidato cha 2 na darasa 1linatumika kama ofisi ya waalimu


Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii Hassan Benzi alikiri idadi hiyo ya wanafunzo kukosa viti na madawati pamoja na vymba vya madarasa akisema jitihada za kukabiliana na tatizo hilo zinaendelea

“Wilaya tumepanga kabla ya mwezi wa sita tutakuwa tumetumia msitu wetu wa mbao wa (SULEDO) kuchana mbao zitakazotumika kuondoa adha ya madawati wilayani Kiteto, tatizo hili siku kiteto peke yake ni nchi nzima”alisema Benzi

Kwa upande wa baadhi ya wanafunzi hao wa kidato cha kwanza walisema adha wanayoipata shuleni ni kubwa, huku wasijue lini wataweza kukaa kwenye madawati wanapokuwa darasani kwani wanakosa usikivu wanapokuwa wanafundishwa kwa kukaa chini

Maoni