Waziri Mkuu asubiriwa kwa mabango Kiteto


                                     Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa


NA. MOHAMED HAMAD 
WANANCHI wilayani Kiteto mkoani manyara wamejiandaa kumpokea kwa
mabango Waziri mkuu Kassimu Majaliwa kuwakataa baadhi ya viongozi
wilayani humo kutokana na mgogoro wa ardhi

Viongozi waliotajwa kukataliwa kwa mabago ni Mkuu wa wilaya ya Kiteto
Kanali Samwel Nzoka, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya
Kiteto, Bosco Ndunguru, Katibu tawala wa wilaya ya Kiteto Nicodemus
John, na Mkuu wa Polisi wa wilaya George Katabazi

Akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani Mkuu huyo wa wilaya
alisema hatoruhusu kufanyika kitendo hicho kwa kuwa kinaashiria kuwa
ni vurugu za kisiasa hi ya wanasiasa kwaajili ya kujijenga kisiasa
kutokana na migogoro hiyo

“Wanasiasa huu sio wakati wa siasa, hiki ni kipindi cha hapa kazi tu,
muda wa siasa umekwisha tuachieni viongozi wenu wa Serikali tufanye
kazi tuachane na siasa,alisema Kanali nzoka wakati akizungumza na
madiwani hao

Alisema taarifa alizonazo kuna watu walioandaliwa kutoka wilaya na
mikoa ya jirani kuja kiteto kutokana na ujio huo wakilenga kuja
kuzomea viongozi hao na kwamba kamwe hawezi kuruhusu hali hiyo

Mkuu wa nchi anapofika kwa wananchi anautaratibu wake wa kuongea nao
hata kama wananchi hawana bango aweza kuzungumza nao ana kwa ana kutoa
kero zinazowasibu alisema

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Waziri Mkuu Majaliwa anakusudiwa kuwasili
wilayani hapo kuongea na viongozi mbalimbali wakiwemo madiwani, wakuu
wa idara, viongozi wa mila wa jamii ya kifugaji (maasai)

Hata hivyo MTANZANIA ilitonywa kuwa Waziri Mkuu pamoja na mambo
mengine anakuja kutoa suluhisho la mgogoro wa ardhi kati ya wakulima
na wafugaji waliohasimiana kwa muda mrefu ambao ulitinga Bungeni zaidi
ya mara mbili

Awali Serikali iliunda kamati mbalimbali pamoja na tume ya maridhiano
iliyokuwa ikiongozwa na Askofu Amos Mhagachi wa kanisa la MENONITE
Dodoma  ya wakulima na wafugaji ambayo ilifanya kazi na kuondoka bila
kutoa taarifa wilayani

Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa ujio wa waziri mkuu Kiteto umelenga
kutoa hitimisho juu ya mgogoro huo ambao ulidumu kwa muda mrefu kati
ya wakulima na wafugaji na ambao ulisababisha watu kupoteza maisha

Mwisho

Maoni