Wafugaji wawatesa wakulima Kiteto

NA Mwanganamatukio
Katika kile kilichoitwa kuwa ni mateso kwa wakulima,yanayotokana na jamii ya kifugaji kwa maksudi kuchunga mashamba yaowilayani Kiteto,wakulima wamesema uvumilivu unakaribia kwisha

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakulima wamesema,kwa muda mrefu wameendelea kuvumilia sasa wamechoka

Kila mara kumekuwepo na malalamiko ya wakulima kupigwa na kulishiwa mazao yao shambani wakidai wanaochinga Ni watoto wadogo

Wamesema kama hoja ni watoto wadogo wameruhusiwa na nani wao kuchunga mifugo mingi ambayo kwao inawashinda nguvu

Wamesema kama Serikali haitakuna na mkakati makini wa kukabiliana na adha hiyo, wajiandae Kuna Mara kwa Mara kusuluhisha pande hizo kwani ugomvi huo hautakwisha

Mwisho

Maoni