Mahakama ya kikatiba nchini Gabon
imethibitisha kuwa Ali Bongo ndiye mshindi wa uchaguzi wa urais
uliofanyika Agosti 27 nchini humo.
Matokeo ya awali yalionyesha ushindi wa Bongo kwa tofauti ndogo ya kura takriban 6000.
Kwa mujibu wa atokeo ya mwisho rasmi yaliotolewa na mahakama ya katiba Bongo alishinda na kura zaidi kutokana na kutobatilisha kura zilizopigwa katika ngome ya kiogngozi huyo Haut-Ogoue.
Hatahivyo kura katika vitu 21 mjini Libreville zimefutiliwa mbali kutokanana ombi la upande wa kampeni ya rais. Na ndio sababu kiongozi huyo amepata asilimia kubwa zaidi katika matokeo ya mwisho.
Upinzani uliwasilisha malalamiko kupinga matokeo ya awali ya uchaguzi na kuiomba mahakama iamrishe kuhesabiwa upya kura hizo, katika eneo hilo la Haut-Ogoue, magharibi mwa Gabon ambapo rais Bongo ana wafuasi wengi.
Kumekuwa na wasiwasi katika mji mkuu Libreville kwamba huenda ghasia zikazuka baada ya mahakama ya katiba kutoa uamuzi wake.
Baadhi ya wakaazi walionekana kununua vyakula na kuweka akiba nyumbani.
Raia mmoja ameiambia BBC: " Nadhani kuna wasiwasi, watu wanataka kuwa salama, wanataka kununua vitu na kusubiria matokeo kwa makini nyumbani, iwao kila kitu kitakwenda sawa itakuwa vizuri"
Maduka mingi yameamua kufunga biashara kukwepa uporaji.
Mapema mwezi huu biashra nyingi ziliathirika.
Maoni
Chapisha Maoni