MKUU wa wilaya ya Hanan’g Sara Msafiri amewatangazia kiama wananchi wanaodaiwa kuwa wavamizi wa shamba la mwekezaji katika kijiji cha Min’genyi kata ya Gehandu na kuwapa masaa 24 kuwa wametoweka ndani ya shamba hilo.
Kiama hicho aliwatangazia wavamizi hao jana wakati akiwahutubia wananchi wa kijiji hicho waliofurika kumsikiliza mkuu huyo wa wilaya ili kufahamu atawafanyaje wavamizi hao wanaotamba kuishinda serikali.
“Natoa masaa 24 kwa waliovamia shamba la mwekezaji kua wameondoka, wasipofanya hivyo wataona kama serikali hii ni dhaifu au siyo dhaifu kama walivyokua wakitamba kua mpaka wasaini kwa dole gumba la mguu.’’Alisema Msafiri
Aidha mkuu huyo amewaonya wananchi ambao wanaowasawishi watu kutoka mikoa mingine wenye uwezo wa kifedha kwa ajili ya kuja kuvamia kuacha tabia hiyo mara moja vinginevyo wataunganishwa na wavamizi wanaokuja na kuwasweka ndani.
“Kama mnafikiri serikali haipo endeleeni kuvamia na kuzigeuza mahakama kua kichaka cha kujificha, awamu hii nitawafunga katika gereza la Babati na hamtatoka kabisa ili mtambue hakuna serikali dhaifu duniani.’’Alisema
Msafiri alisema serikali haitakua tayari kuwavumilia wavamizi wa shamba la mwekezaji kwa Halmashauri inapata mapato yake ambayo yanawasaidia kuendesha Halmashauri.
Licha ya mkuu huyo kuwapiga marufuku watu wanaovamia shamba la mwekezaji amemwagiza mwekezaji wa Ngano Limited Rilash Kalainya kuhakikisha analilima shamba alilopewa na serikali ili wananchi wakaliona alilimwi wakawa na tamaa.
“Kuanzia mwaka huu tutafanya tathimini ya eneo ambalo unalitumia ili kuona kama unalitumia kweli na mwaka kesho hivyo hivyo alafu baada ya hapo tutaandika taarifa na kuituma serikali kuu uendelee kuwepo au lirudishwe mikononi mwa serikali.’’Alisisitiza
Naye mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Hanan’g Braison Kibasa alimtaka mwekezaji huyo kuitendea haki ardhi aliyopewa ili wananchi wasione kua kuna ardhi ambayo inabaki bila kutumiwa na hatimaye kuvamia.
Pia meneja wa shamba la Ngano Limited Rilash Kalainya aliishukru serikali kwa kuja eneo hilo ambalo lilivamiwa na kuaribu vifaa vyake ili kuweza kumpa msimamo wa kumfanya aweze kuendelea kuwekeza hapa nchini.
Kalainya alisema kuharibiwa kwa vifaa vyake kumemsababishia hasara ya zaidi ya shilingi mil. 250 ambapo amesema atakata tama ataendelea kupambana kwa kua serikali kumpa ushirikiano kupitia ushauri na vyombo vya ulinzi na usalama.
Kwa upande wake Shedrack Majengo alisema wavamizi walikuja kijijini hapo watimuliwe kwa kuwa hawana msaada wowote katika kijiji chao na serikali kwa ujumla lakini mwekezaji huyo anawasaidia kutoa huduma za jamii ikiwemo kusaidia ujenzi wa shule na zahanati.
Maoni
Chapisha Maoni