Madiwani Kiteto ndio Suluhisho la migogoro ya ardhi


Mkt wa Halamshauri ya Wilaya ya Kiteto na Diwani wa kata ya Chapakazi Mhe.Lairumbe Mollel kwenye kikao cha madiwani..

Mfugaji Lemomo Moringe kwenye mkutano wa kijiji cha Ilera kata ya Partimbo
Mkulima wa Kijiji cha Ilera katika mkutano wa kijiji unaohusu migogoro


MKUU wa wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara, Tumaini Magessa amesema, suluhisho la migogoro ya ardhi Kiteto ni madiwani kufanya kazi uadilifu na kuacha ujanja ujanja wa kujipatia kipato kwa njia haramu

Akizungumza hayo kwenye kikao cha baraza la madiwani Mkuu huyo wa Wilaya alisema Wilaya hiyo imekuwa ya ahadi (Kaanani) kwa kila kundi kuhamia hapo kutaka ardhi kwaajili ya shughuli za kiuchumi

“Migogoro ya wakulima na wafugaji inatokana na mabadiliko ya tabia ya nchi, kila kundi limekuwa likihitaji kunufaina na ardhi kuzalishia ili aendeshe maisha yake, bila kujali kuwa anaharibu mazingira”alisema DC Magesa

Alisema nafasi ya Diwani ni kubwa kwenye kata yake hivyo akitaka amani iwepo inawezekana , laakini poa akitaka kuchafua hali ya hewa kwa kuwafanya wananchi waishi kwa wasiwasi anaweza

Mkuu huyo wa Wilaya amefikia kusema kauli hiyo kufuatia madiwani hao kuonekana kutokuwa na umoja katika kukabiliana na tatizo la migogoro na kubaki wakiyumba katika maamuzi yao ambayo hayatoi majibu ya tatizo hilo

Wilaya ya Kiteto imetajwa kuwa na majina ya aina tofauti kama vile Somalia, Kossovo, Darfur kufuatia migogoro ya ardhi inayoendelea kujitokea na kusababisha madhara yakiwemo watu kupoteza maisha na wengine vilema vya kudumu

Kufuatia migogoro hiyo, katibu mwenezi wa CCM Christoher Parmet na diwani kata ya Kaloleni alinusurika kifo baada ya kuchomwa mkuki akiwa shambani kwake wakati akizuia mifugo isiharibu mazao yake..

Maoni