MEYA WA DAR AOMBA KAMATI YA BUNGE YA LAAC KUINGILIA MGOGORO WA UDA



MWANDISHI WETU, Dodoma
MEYA wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ameiomba Kamati ya Bunge ya kudumu ya Hesabu za Serikali LAAC kuona namna ambavyo wanaweza kuisaidia ili mgogoro uliopo baina ya Jiji la Dar es Salaam na Kampuni ya Usafirishaji ya Dar es Salaam UDA unamalizika.

Hatua hiyo imekuja baada ya majadiliano ya muda mrefu baina ya wajumbe wa kamati na watendaji wa jiji kushindwa kufikia muafaka juu nani hasa Mmiliki wa kampuni hiyo, sambamba na uwepo wa mwanahisa Saimoni group ambaye ndiye Mwenye hisa nyingi ndani ya Kampuni hiyo.

Meya Isaya alieleza kwamba iwapo kamati hiyo itaingilia Kati Jambo hilo itawezesha pesa ambazo zipo Benki kuu ambazo zilitokana na hisa za shirika hilo kiasi cha billion 5.9 zielekezwe kwenye matumizi mengine kwa ajili ya maendeleo ya jiji la Dar es Salaam.

Alifafanua kwamba pesa hizo hadi sasa bado zipo Benki kuuu na kwamba katika kikao cha baraza la madiwani la Jiji Iililo kaa Aprili 22 mwaka huu lilishauri kwamba pesa hizo zisitumike hadi pale jiji litakapo pata ushauri kutoka kwa mwanasheria Mkuu wa serikali George Masaju.

" Ndugu Mwenyekiti wa kamati , na wajumbe wa kamati hii, jambo hili linatupa wakati mgumu sana, mana pesa ambazo zipo zingefaa kufanya mambo mengine ya Maendeleo, lakini unashindwa, sasa niwaombe tu jambo hili mlichukue tunataka liishe .

Kama baraza liliuliza kuhusu pesa hizo, nakuona kwamba tuombe ushauri kutoka kwa mwanasheria Mkuu wa serikali ,na sisi tulikuwa tunasubiri ushauri kutoka kwake, sasa kwakuwa tayari limeshafika kwenu, tunaomba muliangalie kwa nafasi yenu "aliongeza.

Awali taarifa ya mkaguzo mkuu na mthibiti wa Hesabu za Serikali CAG ilieleza kwamba haitambu mchakato mzima wauuzaji wa shirika hilo la UDA kutokana na kwamba mchakato huo haukuwa wa kihalali na badala yake uliendeshwa kinyemela.

Kwa upande wake wajumbe wa kamati hiyo waliuliza uwepo wa mwanahisa Simon Group ndani shirika hilo, ambapo Mkurugenzi wa Jiji alosema kwamba hafahamu na kwamba hata yeye anashangaa jambo hilo hadi kesho.

"Ndugu Mwenyekiti wa kamati na wajumbe wa kamati hii , nikiulizwa kwanini Simon Group yupo hapa, sina majibu na kwamba mwenyewe naendelea kushangaa hadi kesho kuwepo kwake, sasa sijui,

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo Abdala Chikota alisema kwamba kutokana na majibu ambayo yametolewa , Meya wa Jiji, Katibu Tawala wa mkoa , Mkurugenzi wa Jiji na timu nyingine wafike tena kwenye kamati hiyo Oktoba 28 ambapo waziri wa nchi Ofisi ya Raisi Tawala za mikoa na Serikali za mitaa kufika kwa ajili ya kuangalia namna ambayo wanamaliza jambo hilo.

Chikota alisema anafahamu mlolongo mzima wa jambo hilo na kwamba wanasubiri maelezo ya waziri George Simbachawene ili kuona namna gani ambavyo jambo hilo litamalizika.
Wengine waliowatakiwa kufika kwenye kamati hiyo Mwanasheria mkuu wa serikali George Masaju na msajili wa Hadhina Raurence amafuru.

Posted by Chadema Blogtz at 3:50 AM No comments:

Maoni