Mgogoro wa ardhi Kiteto ni mpaka lini?






NA. MOHAMED HAMAD

Wilaya ya Kiteto iliyopo Mkoani Manyara, imekuwa na migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji, hali iliyosababisha  watu kushindwa kufanya shughuli zingine za maendeleo

Kufuatia migogoro hiyo, baadhi ya idara mbalimbali za Serikali  kama afya,maji na elimu zilionekana kusuasua  kutokana na  migogoro hiyo hali iliyosababisha manunguniko makubwa kwa wananchi juu ya Serikali yao

Hali hiyo ilidaiwa kuwachelewesha sana wananchi kimaendelea, kwa miaka minne mfululizo, wasijue cha kufanya huku baadhi yao wakipoteza maisha na wengine kujeruhiwa wakati wakigombea ardhi, jambo lililosukuma Srikali kuunda tume mbalimbali kuchunguza

Mbali na kupoteza maisha wengi walipata ulemavu wa kudumu, na umaskini kwa kuteketezewa mali zao zikiwemo pikipiki,  mazao, na kuwafanya waishi kwa taabu katika maisha yao, hali iliyoilazimu baadhi ya watumishi wa Serikali kuhamishwa vituo vya kazi

Waliohamishwa ni pamoja na baadhi ya wakuu wa idara, watendaji wa vijiji  na hata wanasiasa kushindwa kurejea katika nyazifa zao wakati wa uchaguzi, kufuatia madai kuwa wamechangia migogoro hiyo

Kwa miaka miwili, Wilaya ya Kiteto ilidaiwa kuwa shwari hali iliyosababisha wananchi wengi kuanza kurejea katika hali zao za kawaida kwa kufanya shughuli zao za kilimo na wengine ufugaji kwa lengo la kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao

Utulivu huo ulisababishwa na tume kadhaa zilizoundwa na aliyekuwa Waziri  Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda, kutaka kujua kiini cha migogoro hiyo na kuitafutia ufumbuzi ambapo waliweza kufanya kazi kwa zaidi ya siku sitini

Kwa mujibu baadhi ya viongozi, walieleza chanzo cha migogoro ya ardhi Kiteto ni kukosekana kwa uadilifu kwa baadhi ya viongozi wa vijiji ambao wametajwa kuuza ardhi kinyemela kinyume cha sheria ya ardhi namba 5 ya mwaka 1999

Akizungumza na wenyeviti wa vijiji 68 pamoja na watendaji wao, Eliakimu Maswi, Katibu Tawala wa mkoa wa Manyara alisema, Serikali imebaini chanzo cha migogoro, na kuwataka watumishi kujipima kama wanaendana na kasi ya magufuli ikiwezekana waache kazi kabla ya kutumbuliw

“Tumebaini kuwa wenyeviti wa vijiji na watendaji wao wamekuwa vinara wa kuuza ardhi, sasa hatuna nafasi ya kuwabembeleza, tutawatumbua na kuwafikisha mahakamani...hatutamwonea haya mwenyekiti tutawakamata DC nakuomba watie ndani bila wonga”

Alisema uwezo wa kijiji kutoa ardhi ni ekari 50, zaidi ya hapo ni wilaya na kiwango cha juu zaidi ni Wizara, inakuwaje mwenyekiti wa kijiji au kitongoji atoe zaidi ya ekari 1,000, 2,000 na hata 5,000 anapata mamlaka hayo wapi mwenyekiti alihoji Katibu Tawala

“DC, Mkuu wa Wilaya naomba sasa tufanye kazi, na wala usisite kumchukulia hatua mwenyekiti wa kijiji, muweke ndani haraka unapoona kuwa amefanya makosa kwa maksudi, kwa kufanya hivyo tutapunguza uhalifu huu”alisema Katibu Tawala Maswi

Kwa upande wa  Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumain Magessa akizungumza na viongozi  wa vijiji alisema, amelazimika kuita kikao hicho cha kazi ili kutaka kuanza ukrasa upya wa kuwavusha salama wanachi wa Kiteto kufanya kazi bila kubughudhiwa

Wakati kukiwa na mikakati hiyo Diwani wa Kata ya Kaloleni, Wilayani Kiteto Mkoani  Manyara, Christopher Parmet (CCM), alinusurika kifo baada ya kuchomwa mkuki na watu wanaodaiwa kuwa ni wafugaji wakati wakiswaga mifugo iliyokuwa imeingia shabani kwake

Tukio hilo limetokea maeneo ya Kisima Kata ya Amei, Wilayani Kiteto, wakati diwani huyo na wafanyakazi wake, Chibundiki Naisoni (54) na Harold Mtalima (56) wakiswaga mifugo iliyokuwa imeingia shambani na kula mazao aina ya mbaazi

 “Baada ya kupigiwa simu na wafanya kazi wangu wa shambani kuwa ng’ombe  wameingia shambani, nililazimika kwenda  na kuwakuta, ambapo tulimpigia simu mwenye mifugo ili aje, lakini alikataa akisisitiza mifugo yake iachiwe mara moja”

Alisema kufuatia hali hiyo alilazimika kuamuru ipelekwe kwa uongozi wa Kitongoji, na wakati wakiiswaga, ghafta lilijitokeza kundi la vijana wa kimasai na kuanza kurusha fimbo na mikuki ambapo hapo waliweza kumchoma mkuki mkono wa kulia na wasaidizi hao kujeruhiwa sehemu mablimbali za miili yao

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa,  alisema, alipigiwa simu na Diwani huyo, aliyekuwa akidai anaishiwa nguvu baada ya kuvuja damu nyingi kwa kuchomwa mkuki  na kuagiza Polisi kwenda kumchukua

Alisema matukio haya awali yalikoma lakini inaonekana kufanywa na wafugaji wa Wilaya za jirani na kutoweka ambapo amedai jitihada za kukabiliana na tukio hilo ni kuwa na daftari la wakazi kila kijiji ili kuwabaini wahalifu hao

Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Emmanuel Papian (CCM) alizitaka mamlaka za Serikali Mahakama na Polisi,  kutimiza wajibu wao ili kukomesha matukio hayo ambayo aliyaita kuwa ni ya kujirudia kwa kutochukuliwa hatua madhubuti

Alisema matukio hayo ni mwendelezo wa mauaji yaliyokwisha kufanyika Kiteto ambapo Wilaya imejipanga kukabiliana na tukio hilo la kihalifu akisisitiza kuwa kila mamlaka zitimize wajibu wao sambamba na wananchi kutoa taarifa mapema kukabiliana na matukio hayo ya kikatili

Mwenyekiti wa wenyeviti 68 Wilayani Kiteto, Salimu Mbwegu, akizungumza kwenye kikao maalumu kilichoitwa mwanzo mpya wa kuirejesha Kiteto yenye amani, chini ya Mkuu wa Wilaya ya Kiteto (DC) Tumaini  Magessa alisema, njia pekee ya kukabiliana na migogoro kila mmoja atimize wajibu wake

“Baadhi ya wenyeviti na wayendaji wao wanalalamikiwa kuhusika katika migogoro ya ardhi, lakini hivi wenyeviti wanalipwa?..na kwanini hawalipwa wanafanyaje kazi za Serikali..tunaitaka Serikali kuwalipa pamoja na kutoa 20% za vijiji ili waweze kujiendesha”

Akijibu hoja hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Tamimu Kambona, aliwahakikishia wenyeviti hao kuwa wameandaliwa malipo yao sambamba na 20% za vijiji japo sio zote ila wapate cha kuanzia katika maendeleleo ya vijiji

Kambona pia aliwaonya baadhi ya watumishi wa Serikali, kuwa niwalevi wa kupindukia kuwa hatowavumilia sheria kali itachukuliwa chidi yao, sambamba na kuwafukuza akidai  utawala huu ni tofauti kwamba hawezi kuendelea kuwavumilia bila kuwatumbua

Mwisho

Maoni