Wajumbe wa kamati ya Siasa Kiteto wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya Kiteto, Tumaini Magessa anayefuata ni Katibu wa CCM Wilaya Pashuwe Shekuwe..
Wanachama wa CCM Kiteto..
Wanachama wa CCM Kiteto..
Na,MOHAMED HAMAD
CHAMA cha mapinduzi CCM,wilayani Kiteto mkoani Manyara, kimewataka
watumishi wa halmashauri ya Wilaya kufanya kazi ili wasitumbuliwe kama
ilivyo katika maeneo mengine.
Akizungumza mbele ya mkuu wa mkoa wa Manyara, Katibu wa CCM Wilayani
Kiteto Mhandisi Pashua Shekuwe, alisema baadhi ya watumishi wamekuwa
kero na kusababisha wananchi kuichukia Serikali yao.
"Mhe Mkuu wa mkoa baadhi ya miradi hapa Kiteto imekuwa kero kutokana
na watumishi kushindwa kuwatunikia ipadavyo wananchi na kuzalisha
malalamiko, hivyo tunaomba sheria kazi zichukuliwa kwa baadhi ya
wazembe
Alisema awali mtu, akitaja kung'olewa jino hospitali ya Kiteto,
mgonjwa analazimika kusafiri kwenda Dodoma,hapo kwanini wananchi
wasichukue Serikali yao".
Hapo ukiuliza utasikia hakuna daktari,vifaa sasa tunataka Serikali
ihakikishe kuwa na watumishi wakutosha, dawa pamoja na vutendea kazi
ili huduma itolewe vizuri kwa wananchi.
Dr. Bendera aliwajulia hali wagonjwa na kuwauliza kama huduma ya afya
zinapatikana ipasavyo ambapo alimwagiza mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya wilaya, Tumimu Kambona kulipa stahili zao Mara moja.
Hawa Abdallah Abdallah (muuguzi)wa zamu aliyekutwa wodi ya wanaume
alisema, kila mara wamekuwa wakitukanwa na wagonjwa kwa kutokuwa na
dawa za kutosha na kutakiwa kwenda kununua kwenye maduka ya watu
binafsi.
"Mhe Mkuu wa mkoa, hapa tunatukanwa na wagonjwa kama watoto kisa
tunawaambia wakanunue dawa nje ya hospitali kutokana na hospitali yetu
kutokuwa na dawa za kutosha"alisema nesi huyo.
Kuhusu malipo ya (overtime)katibu tawala wa mkoa wa manyara Eliakimu
Maswi alimtaka mkurugenzi mtendaji Tamimu Kambona kulipa fedha
hizobmara moja kwakuwa zipo za kutosha.
Kwa upande wa baadhi ya wananchi wilayani Kiteto wamekuwa
na,malalamiko ya muda mrefu kuhusu kauli chafu zinazotolewa na baadhi
ya wahudumu, uhaba wa dawa hali hali hali inayosababisha malalamiko.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kiteto, Tamimu Kambona alikiri
kuwa na fedha hizo na kudai kuwa atalipa kwa muhibubwa taratibu na
mwongozo kutokana na,maelekezo hayo.
Mwisho.
Maoni
Chapisha Maoni