DC Kiteto awataka wenye migogoro kwenda mahakamani

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa..


Na MOHAMED HAMAD
MKUU WA Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Tumaini Magessa, ametaka
migogoro ya ardhi,itatuliwe mahakamani badala ya kukimbilia ofisi ya
mkuu wa Wilaya.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi kwa wasaidizi wa kisheria, chini
ya muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Manyara MACSNET,
amewataka wasaidizi hao kutoa elimu ya sheria kwa umma.

Alisema migogoro mingi inafikishwa kwa DC Mkuu wa wilaya badala ya
mahakamani akisema, hali hiyo imechangia kutomalizika kwa mgogoro wa
wakulima na wafugaji.

Hatuwezi kutatua mgogoro wa ardhi kwa kupeleka mashitaka kwa DC
nendeni kwenye sheria mahakamani, naagiza migogoro hiyo ielekezwe
mahakamani na ninyi wasaidizi wa kisheria saidieni wananchi, alisema
DC Magessa

Akizungumza na wasaidizi 25 wa kisheria, Nemes Iria mratibu wa MACSNET
mkoa wa Manyara alisema awali washiriki,hao walipatiwa mafunzo ya
usaidizi wa kisheria ili wawe msaada kwa umma ambalo sasa wanaenda
kuusaidia umma katika masuala mbalimbali yakiwemo ya ukiukwaji wa
sheria.

"Mkuu wa Wilaya hapa tayari una wasaidizi 25 wa kisheri ambao naamini
watakuwa msaada mkubwa kwa wananchi, kwani moja ya kazi kubwa
watakayofanya ni kutoa msaada wa kisheria

Akizungumza kwa niaba ya wasaidizi hao wa kisheria mwenyekiti wa
mashirika yaliyoungana kufanya kazi ya usaidizi wa kisheria, Mwadawa
Ally alishukuru wadau na shirika la CELG chini ya wafadhili wa LSF kwa
kuwezesha elimu kwa mashirika hayo

Alisema elimu hiyo imefika wakati mwafaka ambao Kiteto inakabiliwa na
migogoro ya ardhi ambayo imesababisha watu kupoteza maisha na kufanya
wasigikie maendeleo tarajiwa.

Mwisho

Maoni