Kiteto wateketeza dawa za kulevya



Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, (DC) Tumaini Magessa akiwa katika harakati za kuteketeza madawa ya kulevya aina ya bangi.. 
Kamati ya ulinzi na usalama chini ya mkuu wa Wilaya ya Kiteto DC Tumaini Magessa wakiwa katika harakati za kuteketeza madawa ya kulevya
Shehena ya madawa ya kulevya, bangi ikiandaliwa kwenda kuteketezwa Kiteto..


Mkuu wa Wilaya ya Kiteto DC Tumaini Magessa, akisimamia kupakia pombe moshi aina ya gongo kwenye zoezi la uteketezaji wa madawa ya kulevya ambapo jumla ya lita 1,080 ziliteketezwa..
Shehena ya madawa ya kulevya bangi ikiandaliwa kuteketeza kiteto..



DAS Kiteto Stephano Ndaki, katika zoezi la uteketezaji madawa ya kulevya..
 Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, DC Tumaini Magessa, akiwasha moto kuteketeza madawa ya kulevya aina ya bangi..
 Mkuu wa Wilaya ya Kiteto DC Tumaini Magessa akicteketeza Bangi..

Mkuu wa Kituo cha Polisi Kiteto, Patrick Kimaro (SABASITA) na Katibu tawala wa Kiteto Ndaki Stephano wakidhibiti moto zoezi la kuteketeza madawa ya kulevya..
Mkuu wa Wilaya DC Tumaini Magesa mwenye suti nyeusi akiongoza zoezi la kuteketeza mpombe haramu aia ya gongo..


 Na,MOHAMED HAMAD.

MKUU wa wilaya ya Kiteto,Tumaini Magessa, ameongoza zoezi la
kuteketeza dawa za kulevya aina ya bangi, kg 250, na pombe haramu aina ya gongo
lita 1,080 pamoja na voroba feki 200.

Hatua hiyo imetokana na mapambano ya dawa za kelevya yanayoendelea
hapa nchini, ambapo hivi karibuni jeshi la Polisi lilifanya msako na
kubaini shamba la bange maeneo ya Emboley Murtangos.

Alisema katika msako huo walikamata pombe haramu aina ya gongo
lita 1,080 ambapo baada ya sheria za kimahakama kufanyika
waliteketeza kama njia ya kutokomeza ulevi pamoja na dawa za kulevya.

Akizungumza katika mkakati wa kutokomeza dawa za kulevya,na ulevi wa
pombe haramu (gongo) akiwa na askari polisi na hakimu mkazi wa wilaya
ya Kiteto, Elimo Masawe,DC Magessa, aliwataka kila mtu kwa nafasi yake
kushiriki vita hiyo.

"Ushindi wa vita unatokana na ushirikiano..nimeamua kukutana nanyi
tuweke mikakati ya namna ya kukabiliana na zoezi hili ambalo Rais wetu
ametoa maelekezo kupambana nalo,polisi , mahakama, mnawajibi wenu
katika hili.

Mkuu wa kituo cha Polisi Kiteto,Patrick Kimaro (Sabasita) katika
mchango wake aliomba zoezi hilo lifanyike kwa uzalendo tena kwa kuunga
mkono kwa dhati jitihada za Rais kwa kuwa ni agizo bila kisingizio
chochote

"Mhe mkuu wa wilaya hapa tutafanikiwa endapo Jeshi la polisi
na,mahakama tutakuwa na ushirikiano katika vita hii..na ninaamini kwa
tulivyojipanga mhalifu hana nafasi"

Hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya, Elimo Massawe, aliwataka polisi
ili kufanikisha zoezi hilo baada ya kukamata mhalifu wahakikishe
wanafuata taratibu zote za kiushahidi mahakamani

Alisema ushahidi ndio unaofunga mhalifu, hivyo alisema mchango wa
mahakama katika zoezi hilo utaonekana akisisitiza kutenda haki katika
zoezi hilo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya ya Kiteto (DC)Tumaini Magessa alisema,
Kiteto ni moja ya eneo ambalo linazalisha madawa ya kulevya aina ya
bange huku mirungi ikisafirishwa kutoka mikoa ya jirani kuja hapa.

Mwisho.



Maoni