Madiwani Kiteto wapitisha bajeti ya bil 37.6


                                                         Madiwani wa Kiteto..

Na, MOHAMED HAMAED

BARAZA la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, limepitisha mapendekezo ya bajeti  ya tsh mil. 37,634,602,281 yatakayotumika  kwa mwaka 2017-2018 kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto, Jemes Kionaumela, alisema tofauti ya bajeti ya mwaka 2017 na mapendekezo ya 2018 ni bil 10 ambapo mwaka 2016-2017 ilikuwa bil 27 na mwaka 2017- 2018 ni zaidi ya bil 37.6 ambapo alitaja vipaombele kuwa ni kuboeresha mapato ya ndani,kufanya mpango ya matumizi bora ya ardhi


Vingine ni utoaji wa elimu bure ya msingi na sekondari,ununuzi wa gari moja kwaajili ya shughuli za halmashauri,ununuzi wa trekta mbili kwaajili ya kuzolea taka ngumu, kupeleka 20% vijijini, kutoa 10% kwa vijana na akinamama katika mapato ya ndanI

Kukamilisha miradi viporo,kuendelea na awamu ya tatu ta jengo la halmashauri ya wilaya,  ajira ya watumishi wapya na upandishaji vyeo, utawala bora, stahili za watumishi,kusimamia amani na utulivu,kutenga maeneo ya uwekezaji, na kufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo .

Changamoto kwa mwaka 2016-2017, Lairumbe Mollel mwenyekiti wa halmashauri hiyo alitaja kuwa ni kuchelewa kutolewa kwa ruzuku ya miradi ya maendeleo, kutopitishwa sheria ndogo za ukusanyaji wa mapatona mamlaka husika, umbali kutoka makao makuu ya wilaya na makao makuu ya mkoa inayowalazimi kupitia wilaya ya Kondoa na umbali wa maeneo ya kata na vijiji kutoka makao makuu ya halmashauri

Kwa upande wa Christopher Parmet diwani wa kata ya Kaloleni (CCM) alisema kama mvua hazitanyesha kama inavyoonekana  hadi February mwaka huu kutonyesha mvua bajeti ya mwaka 2017-2018 itaathiriwa kutokana na halmashauri kuwa na vyanzo tegemezi vikuu viwili ambavyo ni ushuru wa mazao na mifugo

Baadhi ya wananchi waliozungumzia bajeti hiyo waliitaka Serikali kutoa fedha kwa wakati ili ziweze kutekeleza miradi ya maendeleo hali inayoelezwa kuwa kupanga bajeti ya kutekeleza miradi inachelewesha maendeleo ya wananchi kwa ujumla

Mwisho.

Maoni