MVIWATA Kiteto wabaini mradi wa umma kuuzwa.

                                                  Mwezeshaji Thomas Lizer akifafanua jambo..
                         Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Lairumbe Lebabu Mollel..

                                                             Mwezeshaji Thomas Lizer
                                        Robarth Urassa,afisa Kilimo wa Wilaya ya Kiteto..

                        Wajumbe wa kamati ya PETS ya MVIWATA Kiteto wakifuatilia jambo...
                                   Diwani wa kata ya Dosidosi, Hassani Benzi akifafanua jambo...
                                                 Mwenyekiti wa PETS Bw  Apolo Chamwela akiwasilisha taarifa..




Na, MOHAMED HAMAD, KITETO

MTANDAO wa vikundi vya wakulima Tanzania, MVIWATA wilayani Kiteto mkoani Manyara, umeibua ubadhirifu wa Tsh 6.9 mil, zilizotolewa na halmashauri kwaajili ya kununua mashine ya kukamlia alizeti kwa kikundi cha wakulima wa kata ya Dosoidosi cha masahiyo.

Apolo Chamwela, mwenyekiti wa timu ya ufuatiliaji na uwajibikaji umma (PETS) ya MVIWATA wilayani Kiteto, akiwasilisha mrejesho wa taarifa ya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma mradi wa kilimo kijiji cha Dosidosi alisema, wamebaini ubadhirifu katika kikundi hicho.

Alisema kikundi kilipokea fedha kutoka Halmashauri kwaajili ya utekelezaji wa mradi wa mashine ya kukamua alizeti wa thamani ya Tsh 6.9 mil, wenye vifaa kama.. (screw Oil Press-6YC 9SA, Injini 1-24 HP, chujio 1 na chasis bolts vyote vya thamani hiyo

Alisema mashine hiyo ya alizeti haipo, Jengo la mashine halikukamilika, huku likionekana kuchakaa, na huduma ya ukamuaji mafuta ya alizeti hazipo, huku kukiwa na wazo la kuuzwa kwa jengo hilo kutokana na kutokuwepo kwa mashine hiyo ya alizeti


Katika hatua hiyo alisema usimamizi mbovu wa miradi, ushiriki na ushirikishwaji duni wa wananchi husika na kutokuwepo kwa uwajibikaji wa wananchi, kumechangia mradi wa mashine ya kukamua alizeti kufanyiwa hujuma na wanakikundi hicho

Mradi mwingine ambao umedaiwa kusuasua ni josho la kuogeshea mifugo katika kijiji cha Esugta, kata ya Dosidosi ambao uliogharimu mil 15, nao ulifadhiliwa na halmashauri kupitia PARDEP, huduma haipatikani kutokana na jengo kutokamilika

Hassani Benzi, diwani wa kata ya Dosidosi (CCM) akizungumza kwenye kikao hicho cha wadau wa maendeleo mjini Kibaya alikiri kuwa mashine ya kukamulia mafuta ya alizeti iliuzwa katika mazingira ya kutatanisha

“Bila kumumunya maneno..ile mashine iliuzwa, hawa wezetu wa PETS ya MVIWATA Kiteto, niwashukuru sana kwa kuibua haya kwani huenda likafuatiliwa kwa kina kwani ule ni mradi wa jamii sio wa baadhi ya watu wachache ”alisema diwani Benzi

Kwa upande wake Christopher Parmet diwani wa kata ya Kaloleni (CCM), alisema miradi mingi imeonekana kudhorota kutokana na ujanja ujanja wa baadhi ya viongozi wa vikund, hii ni dili.. namtaka mkurugenzi mtendaji kuwakamata wahusika na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria

Thomas Laizer mwezeshaji katika mrejesho huo wa taarifa alisema, kuna kila sababu ya viongozi wa Serikali kujipima katika kazi zao, akidai kudhorota kwa miradi hiyo, kunatokana na kutowajibika kwa pande zote mbili wataalamu pamoja na wananchi

“ Kwa hili wataalamu wangu wa kiteto mmeteleza..mlipaswa kuwa washauri wakuu katika miradi hii..mpaka wananchi wanauza mradi wa jamii mko kimya mnadhani kuna usalama hata katika miradi mingine?”alihoji Thomas

Abdallah Bundallah diwani wa kata ya Songambele (CCM) alisema hakuna  sababu ya diwani kujiita mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata wakati miradi iliyopo kwenye kata yake inadorora..

“Unapata wapi ujasiri wa kujiita mwenyekiti wa maendeleo ya kata wakati wananchi wanauza miradi ya umma.. wewe upo huwezi kuzuia unakazi gani hapo?” alisema diwani Bundara huku akionekana kukerwa na tabia hiyo

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Lairumbe Mollel (CCM) katika mjadala huo alikiri kudhorota kwa miradi ya maendeleo akisema imetokana na jamii kutoshiriki kikamilifu, huku baadhi ya watumishi wa Serikali wakiwa tatizo

Mwisho

Maoni