RC Manyara aagiza fedha za TASAF wapewa walengwa

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dr, Joel Nkaya Bendera..
 Walengwa wa TASAF Kiteto wanaopaswa kusaidiwa..

 Walengwa wa TASAF Kiteto wanaopaswa kusaidiwa..

MOHAMED HAMAD

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dr. Joel Nkaya Bendera, amemwaagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Tamimu Kambona , kuhakikisha fedha walizopewa kaya ambazo sio maskini zinarejeshwa

Akizungumza na wananchi wa kata za Magungu na Engusero, Dr. Bendera amesema lengo la Serikali ni kupunguza makali ya maisha kwa kaya maskini kwa kuwapa fedha keshi, tofauti na awamu zilizopita kupitia mradi wa jamii TASAF

Kufuatia lengo hilo Dr. Bendera amebaini kaya 7 kata ya Engusero, kati ya 29 Wilayani humo na 700 Mkoani Manyara,  sio walengwa na wanapokea ruzuku ya Serikali kinyume na matakwa na kuagizo ya Serikali

Kwa mujibu wa Tamimu Kambona, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kiteto, amekiri kuwepo kaya ambazo hazistahili kupokea fedha  hizo na kudai kuanza kufuatilia fedha hizo ili ziweze kupewa walengwa

Alisema wanaobaini kaya maskini ni wananchi wenyewe kulingana na aina ya umaskini katika eneo husika hivyo waliokuwa wanapata ambao hawastahili walipitishwa na mkutano mkuu wa Kijiji

Mwisho

Maoni