Mifugo ya Kiteto, yanufaika na maji yaliyochimbwa na shirika la Elewa Afrika.. 
Mkuu wa wilaya ya Kiteto Tumaini Magessa akifafanua jambo kwenye uzinduzi wa mradi wa maji chini ya shirika la Elewa Afrika, mpakani mwa vijiji cha Orkitikiti na Lengatei Kiteto Manyara..
 Mratibu wa shirika la Elewa Afrika Fadhili Magogwa, akimkabidhi mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa, taarifa ya mradi..
 DAS Kiteto, Ndaki Stephano akifafanua jambo kwenye uzinduzi wa mradi wa shirika la Elewa Afrika kata ya Lengatei Kiteto Manyara Tanzania.. 
 Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Tamimu Kambona akifafanua jambo..
 Kamati ya ulinzi na usalama kiteto..

Wananchi wa kata ya Lengatei Kiteto Manyara Tanzania..

Mkuu wa wilaya ya Kiteto katika picha ya pamoja..

 Na, MOHAMED HAMAD

 WANANCHI wa kata ya Lengatei wilayani Kiteto mkoani manyara, wameanza kunufaika na shirika la Elewa Afrika, kwa kuchimbiwa kisima cha maji chenye uwezo wa kutoa lita 19,000, kwa saa

Akizungumza mbele ya mkuu wa wilaya ya Kiteto, mratibu wa shirika hilo Fadhili Magogwa, alisema huo ni mwanzo wa shirika kuanza kusaidia wilaya ya Kiteto  wakianza na kata hiyo, ikiwa lengo ni kutawanya huduma hiyo wilayani Kiteto..huku mkuu wa wilaya akiliomba shirika hilo kuendelea kuisaidia wilaya ambayo kwa sasa inamatatizo ya maji



KWA HISANI YA mwanganamatukio..

Maoni