Wafugaji 200 toka Kilindi waomba hifadhi Kiteto

                                              Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Tumaini Magessa..


Na, MOHAMED HAMAD

ZAIDI wa wafugaji 200 wa jamii ya  maasai kutoka wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga, wameomba hifadhi wilayani Kiteto kuhofia maisha yao kutokana na mgogoro wa ardhi kati ya wakulima na wafugaji Wilayani Kilindi.

Akizungumza na MTANZANIA mkuu wa wilaya ya Kiteto (DC) Tumaini Magessa alisema, amelazimika kukutana na wafugaji hao mpakani mwa Kiteto na Kilindi na kuongea nao ambapo ameagiza wananchi kuwapokea na kuwapa msaada

" Kwa hali niliyowakuta baada ya kupewa taarifa, nimewaomba wananchi waliopo mpakani katika  Kijiji cha Lembapuli na hata Mesera, wawapokee wakati Serikali tunajipanga namna bora ya kuwasaidia"

Mbali na msaada huyo naendelea kuwasiliana na mkuu wa Wilaya ya Kilindi juu ya wananchi hao kutoka kwake, kuona namna bora ya kuwasaidia, sambamba na kutafuta suluhu ya mgogoro wa wakulima na wafugaji

Kwa upande wa diwani wa kata ya Loolela Kosey Lehinga (Chadema) alisema pamoja na wananchi kuwa na haali ngumu ya kiuchumiamewataka wawe na roho ya kibinadamu kuwapokea wananchi hao na kusema kuna kila sababu ya Serikali kufanya haraka ya kuwasaidia

"Hiki kipindi ni cha njaa kila mtu analia..sasa unapoongeza mzigo mwingine tofauti na uliobeba ni hatari zaidi, tunaiomba Serikali ya wilaya na hata mkoa kuona haja ya kuwasaidia" alisema Lewhingaa

Misaada inayotakiwa hivi sasa ni pamoja na chakula malazi dawa, ikizingatiwa wengi wao ni watoto wadogo na wanawake, huku wanaume wakibaki maeneo ya kilindi kulinda mali zao

MWISHO


Maoni