Watoto wa kifugaji Kiteto wakosa haki ya kikatiba


                                    Mtoto wa jamii ya kifugaji, maasai akichunga mifugo..
                           Baadhi ya wanajamii ya kifugaji, maasai wakiwa kwenye kikao..
                            Akinamama wa jamii ya kifugaji katika shughuli zao za kila siku..
             MKUU wa Wilaya ya Kiteto, mkoani Manyara (DC) Tumaini Magessa, akisisitiza jambo..



NA. MOHAMED HAMAD
PAMOJA na Serikali kwa kushirikiana na mashirika ya umma, kupiga vita ajira za utotoni…baadhi ya makabila, Wilayani Kiteto mkoani Manyara, yamedaiwa kuwatumikisha watoto wao kwa kuchunga mifugo.

Katika kazi hiyo watoto hao hukosa haki ya kikatiba ya kupata elimu, huku kukiwa na sheria za kuwalinda na ambazo kwa sasa zimedaiwa kutowasaidia kupata haki hiyo.

“Ninachojua Serikali inatakiwa kila mtoto mwenye umri wa Kwenda shule akasome, lakini inakuwa kinyume chake hapa Kiteto, jamii ya kifugaji wengi wa watoto wao hawaendi  shule badala yake wanachunga ng’ombe” Alisema Mohamed Bakari Mahusi..

 Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, Wilayani Kiteto, imeelezwa kuwa chanzo cha migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo ilisababisha maafa ni watoto hao kuachia mifugo shambani na kuharibu mazao ya wakulima...

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto (DC)Tumaini Magessa, akizungumza na mwanganamatukio aliapa kushughulika na wazazi wanaowatumikisha watoto kwa kuchunga mifugo badala ya kuwasomesha..

Maoni