Vyeti feki vyaathiri Meimosi Kiteto..

DC. Tumaini magessa wa Kiteto, akifafanua jambo sikukuu ya meimosi Kiteto 2017..
 Sikukuu ya wafanyakazi Kiteto..
 Zahara Godah akisoma risala ya watumishio sikukuu ya wafanyakazi Kiteto..
 Katibu wa ccm Kiteto Pashue Shekuwe katikati akifuatilia sikukuu ya wafanya kazi ..
 Kamati ya ulinzi na usalama Kiteto wakifuatilia sikukuu ya wafanya kazi....

Wafanyakazi wa idara ya afya kiteto wakifuatilia hutuba sikukuu ya meimosi..
 Mkuu wa wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa, kulia na Lairumbe Mollel Mkt wa Halm ya kiteto wakifuatilia jambo sikukuu ya wafanyakazi..








Baadhi ya viongozi wa chama cha walimu Kiteto wakiuza bidhaa zao..
 Ndaki Stephano DAS Kiteto akimwonyesha bidhaa inayouzwa na CWT Kiteto, Mkurugenzi wa Kiteto..


Mwenyekiti wa Halm Lairumbe mollel akipewa cheti cha utumishi bora..


Diwani Zamzam Ramadhani akimvisha taji mkt wa Halm Lairumbe Mollell..\


 NA. MOHAMED HAMAD
VYETI feki kwa baadhi ya watumishi wilayani Kiteto mkoani manyara, vimedaiwa kuathiri sherehe za watumishi Meimosi wilayani Kiteto mkoani manyara, baada ya wengi wao kutohudhuria

Akizungumza wakati wa maandalizi ya maandamano, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Tamimu Kambona, alisema wengi wa watumishi wamekata tamaa kwa wenzao kudaiwa kuwa hewa

" Wapo waliopata matatizo baada ya kuambiwa kuwa ni hewa (wamelazwa) Hosp, hili kwetu sisi ni pigo, hasa ikizingatiwa kuwa wilaya ya Kiteto ilikuwa na uhaba wa watumishi toka mwanzo

Najua Serikali ina nia njema katika kazi hiyo, siwezi sema kuwa kufanya hivyo ni kosa ila kwa kiteto idadi ya watumishi inazidi kupungua baada ya hawa 65 kutakiwa kuondolewa..

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara DC Tumaini Magessa alisema, ili mtumishi aweze kujitafsiri katika Serikali ya awamu ya tano, lazima aonyeshe kuwa amesomea wapi sambamba na kuonyesh cheti chake..

Naye Paulo Gwacha mwenyekiti wa Chama cha walimu Kiteto alisema, majonzi yametanda kwa waalimu, kufuatia wenzao kutakiwa kujiengua kutokana na sakata la vyeti, na kuongeza kuwa kwa sasa hali itazidi kuwa mbaya kiteto kwa uhaba wa watumishi..

Hata hivyo sherehe za meimosi Kiteto, zimeonekana kuhudhuriwa na watumishi wachache huku baadhi yao wakipongezwa kwa kufanya kazi nzuri na wengine kupata zawadi kwa kustaafu salama,

Katika Sherehe hizo Mkurugenzi mtendaji wa Halamshauri ya Wilaya ya Kiteto Tamimu Kambona, alitunukiwa cheti cha ufanyakazi bora kutokana na kujitoa kwake kufanya kazi kwa bidii siku zote..

Mwisho







Maoni