Kiteto waungana kuazimisha siku ya mtoto wa Afrika 2017

 Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, DC. Tumaini Magessa, mwenye suti, nyeusi ndani ya maombi siku ya mtoto wa Afrika, Kiteto mwenye mic ni mchungaji katika maombi hayo..
Wanafunzi wanaohudumiwa na Compassion Tanzania Kiteto, katika maazimisho ya siku ya mtoto wa Afrika
NA. MOHAMED HAMAD

Wilaya ya Kiteto, mkoani manyara, imeungana na wilaya zingine hapa nchini kuazimisha siku ya mtoto wa Afrika, ambapo pamoja na mambo mengine wamekemea mimba za utotoni, ukeketaji na utoro shuleni

Akizungumza na mamia ya wanafunzi hao Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa, ameitaka jamii wilayani hapo kuacha tabia za kuwapa mimba wanafunzi wa kike na kuwakatisha masomo huku wakiume wakiajiriwa kufanya kazi kinyume cha sheria
Alisema zaidi ya wanafunzi 500 wa jamii ya kifugaji, wamasai na wakulima  wamekamatwa na kuandikishwa shule chini ya mwamvuli wa serikali huku 200 wakiwa wamepachikwa mimba na kuacha shule

Amewapongeza waalimu na wanafunzi wa Compassion Tanzania kwa maonyesho mbalimbali akisema Serikali iko nao bega kwa bega kuhakikisha wanafunzi wanapata haki yao ya kikatiba ya elimu

Baadhi ya wananchi wamelaani kiteto za kukatishwa masomo wanafunzi na kuitaka Serikali kuingilia kati kuokoa hali hiyo ili kuondokana na taifa la watu wasiojua kusoma na kuandika

Sherehe hizo zimeandaliwa na umoja wa makanisa chini ya shirika la Compassion Tanzania, ambapo zaidi ya wanafunzi 1000 walishiriki katika maadhimisho hayo..

TAARIFA ITAENDELEA...

Maoni