Ajali ya basi yajeruhi 20 Manyara

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Celestino Mofuga ( mwenye nguo nyekundu) akiwa eneo la tukio ambalo mabasi mawili yamegombana kisha moja kutumbukia darajani
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Celestino Mofuga, akiwa eneo la tukio
Mmoja wa majeruhi wa ajali ya basi kugongana Mbulu ambaye jina lake halikufahamika mapema akipata matubabu katika hospitali ya Mbulu

Ajali ya basi yajeruhi 20 Manyara

Na MOHAMED HAMAD MBULU
JUMLA ya abiria 20 wamenusurika kifo kutokana na ajali ya mabasi kugongana kisha moja kutumbukia darajani wakati yakifanya safari zao za kutoka wilayani Mbulu mjini na vijijini mkoani Manyara

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili, mkuu wa wilaya ya Mbulu, Celestino Mofuga, alisema ajali hiyo imesababishwa na madereva wotw wawili kushindwa kumudu mabasi hayo kutokana na mwendo kasi

Alisema kutokana na ajali hiyo jumla ya abiria ishirini kutoka katika mabasi hayo wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mbulu na watatu wamepelekwa hospitali ya Hydom kwaajili ya matibabu zaidi

“Mabasi yalikuwa na mwendokasi, madereva walishindwa kuyamudi na kugongana katikati ya darajani, kisha moja kudumbukia darajani”, alisema (DC) Mofuga, Mkuu wa Wilaya ya Mbulu

Alisema mabasi yanayofanya shughuli za usafirishaji wa  abiria ni chakavu,  na hata kama yatapigwa marufuku itakuwa  ni kusimamisha huduma hiyo ingawa mara nyingi wamiliki hutakiwa kufanya matengenezo mara kwa mara

Kwa mujibu wa mmoja wa wahudumu wa hospitali ya wilaya ya Mbulu ambaye hakutaka kutaja majina yake gazetini, alikiri kuwahudumia majeruhi hao na kusema jitihada za kuokoa maisha ya abiria hao zinaendelea

Alisema wengi wao wameumia sehemu mbalimbali za miili yao kwa kupata majeraka mikononi na miguuni pamoja na vichwani  wakati wa ajali hiyo  

Michael Dohah shuhuda wa ajali hiyo alisema tukio hilo lilitokana na mwendo kasi pamoja na ufinyu wa barabara katika eneo hilo jambo ambalo lilisababisha madereva kushidwa kumudu agari yao

“Tuna tatizo kubwa la ubovu wa barabara, hali inayofanya magari yenye hadhi na mazuri kutofanya shughuli zao humu na kulazimika kutumia magari mabovu ambayo mara nyingi huhatarisha maisha yetu kama ilivyotokea”alisema

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Manyara, Francis Masawe hakupatikana kuzungumzia tukio hili, pamoja na kwamba simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa, huku maafisa wengine wakikiri kutokea ajali na kudai wao sio wasemaji

Mwisho



Maoni