LHRC uelewa mdogo wa kisheria kwa wananchi unanyima haki

 Rodrik Maro, Mwanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) akimsikiliza mteja wake Bw. Gabriel Neeli Polpukot wa Kijiji cha Lerug Kata ya Kijungu Wilayani Kiteto mkoani Manyara Bw.Gabriel
Rodrick Maro, Mwanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) akifafanua jambo mbele ya wananchi wa Kijiji cha Lerug ambao hawapo pichani..
Mwenyekiti wa Kijiji cha Lerug Bw. akifafanua jambo mbele ya wananchi wake baada ya kutembelewa na wanasheria wa Kituo cha sheria na Haki za Binadamu LHRC kijijini kwake..
Mwanasheria Evance Kaijage wa LHRC akitoa elimu ya kisheriambele ya baadhi ya wananchi wa kijiji cha Lerug Wilayani Kiteto mkoani Manyara..
Mwanasheria Janeth Kazimoto wa LHRC, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lerug baada ya kufika wilayani Kiteto mkoani Manyara..
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Lerug wakifuatilia mkutano wakiwa na wanasheria wa LHRC katika kijiji cha Lerug Kiteto Manyara..
Bw. Gabriel Neeli Polpukot wa Kijiji cha Lerug Kata ya Kijungu Wilayani Kiteto mkoani Manyara, akiwa katika usuluhishi wa tatizo kimila katika kijiji cha Lerug Kiteto

Wanasheria wa LHRC wakimsikiliza Bw. Gabriel Neeli Polpukot wa Kijiji cha Lerug Kata ya Kijungu Wilayani Kiteto mkoani Manyara
Baadhi ya vijana wa jamii ya kifugaji maasai wakisima vitabu vyenye taarifa mbalimbali zilizoandikwa na LHRC




Na MOHAMED HAMAD
UELEWA mdogo wa wananchi wilayani Kiteto mkoani Manyara, kuhusu elimu ya kisheria unawanyima haki mbalimbali za kisheria wanapofikishwa kwenye mamlaka za kisheria.

Hayo yameelezwa na wakili msomi, Janeth Kazimoto wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), alipokuwa akitoa msaada wa kisheria kwa wananchi mjini Kibaya.

Alisema wananchi wengi wanapoteza haki zao kutokana na uelewa mdogo wa kisheria na kuwataka kuomba msaada wa kisheria ili waweze kupata haki zao.

“Ni vyema wananchi wakaomba msaada kutoka kwa watoa huduma za kisheria, hususan mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ambayo yanajihusisha na masaada wa kisheria yaliyopo Kiteto pamoja na wasaidizi wa kisheria ili waweze kutetea haki zao.”

Alisema kwa kufanya hivyo kutawanusuru kulinda haki zao tofauti na ilivyo sasa kuwa wanachangamoto za kisheria na hata lugha za kimahakama

Kwa upande wake Rodrick Maro, mwanasheria wa LHRC alisema kutokana na matatizo mbalimbali yanayowakabili wananchi, jopo la wanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu limeamua kutoa msaada wa kisheria wilayani hapa.

Alisema wilaya ya Kiteto inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo migogoro ya ardhi, ndoa, mirathi, ukatili wa kijinsi, ukeketaji,ubakaji na kulawiti; vipigo kwa wanawake, na ndoa za umri mdogo.

Naye Mwadawa Ally, mratibu wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto, alikiri kuwepo kwa ukatili, hususan wa kijinsia akisema jamii wilayani humo bado inahitaji elimu zaidi.

“Jamii ya kifugaji ya Wamaasai haijaona umuhimu wa kumthamini mtoto wa kike na kumuona kama bidha ya kuuza ili wapate mali kama ilivyokuwa mifugo.”

Kuna vipigo kwa jamii hiyo pamoja na elimu kutolewa bado hali hiyo inajirudia kutokana na kutowaamini wataalamu kwa kuwataka mambo yao yaelezwe na viongozi wao wa mila (Malaigwanani).


MWISHO




Maoni