Madiwani Kiteto wapata makamu mwenyekiti mpya wa halmashauri

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto, Tamimu Kambona akimkaribisha mkt wa halmashauri ya wilaya Lairumbe Mollel kufungua kikao cha baraza la madiwani
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Lairumbe Mollel akifungua kikao cha baraza la madiwani Kiteto
Makamu mwenyekiti mpya wa halmashauri ya Kiteto Hassan Benzi akishukuru madiwani kumchagua kuongoza kwa mwaka mmoja
Mkt wa halmashauri ya wilaya Lairumbe Mollel akisisitiza jambo kwenye kikao cha madiwani Kiteto
Madiwani wa Kiteto wakifuatilia kikao cha madiwani kilichoketi hivi karibuni mjini Kibaya
Mbunge wa Kiteto Emmanuel Papian kushoto wakiteta na Mkuu wa Wilaya Tumaini Magessa kwenye kikao cha badiwani..
Mwasigwa Kimosa kushoto diwani Kiteto akifuatilia kikao cha baraza la madiwani
CC Athumani Kituru kulia akifuatilia kikao cha baraza la madiwani
Viongozi wa Jukwaa la vijana Kiteto wakifuatilia kikao cha baraza la madiwani
Wananchi wa Kiteto wakifuatilia kikao cha baraza la madiwani Kiteto
Aliyekuwa makamu mwenyekiti wa halm ya Wilaya ya Kiuteto Yahaya masumbuko akifurahia jambo kwenye kikao
Katibu Tawala wa wilaya ya Kiteto Ndaki Stephano kulia akifuatilia kikao cha madiwani
Afisa ardhi Gurisha akifuatilia kikao cha madiwani Kiteto..
Madiwani wakipiga kura ya kumchagua makamu mwenyekiti wa halamshauri ambapo alichaguliwa hassan Benzi
DC Tumaini Magessa kushoto akifuatilia jambo kikao cha madiwani Kiteto




NA MOHAMED HAMAD
BARAZA la madiwani Kiteto mkoani manyara limeketi na kumchagua Hassan Benzi kuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo kuongoza kwa mwaka mmoja baada yaYahaya Masumbukuko kuongoza kwa mwaka mmoja uliopita.

Akiwashukuru madiwani hao Hassan Benzi mamaku mpya wa mkt wa halm aliomba ushirikiao kwa viongozi hao wa siasa ili aweze kutimiza ndoto zake katika nafasi hiyo akisema ana deni kubwa kwa wananchi kuwaletea maenddeleo ya kweli

Katika kikao hicho suala la barabara kutoshughulikiwa na halm ya wilaya na wakala TARURA kuchukua nafasi hiyo lilichukua sura mpya baada ya madiwani kupata hofu ya barabara kutotengenezwa kwa kiwango kinachotakiwa 

Elia Dengea, na Mussa Briton ni madiwani walionyesha hofu hiyo wakisema utaratibu huo utafanya barabara nyingi zisitengenezwe kwa kutokana na mfumo huo ambao hauonyeshi wapi madiwani wanapoweza kukutana na TARURA katika vikao vya halm

Mkurugenzi mtendaji wa Halamshauri ya Wilaya ya Kiteto Tamimu Kambona aliwatoa hofu madiwani kwa kuwataka kuwe na imani na Serikali kuwa ina nia njema kuboresha huduma hiyo kwani wakurugenzi walionekana kuzidiwa majukumu hivyo sasa wamepunguziwa kazi

Katika hatua hiyo suala la mgogoro wa ardhi lilichukua sura mpya baada ya diwani wa kata ya Kijungu Mandalo Abdilah kuhoji kutotatulika mgogoro wa ardhi kati ya vijiji vya Kijungu, Amei na Lolela ambao ni wa muda mrefu

Alisema wananchi wa kijiji mama cha Kijungu kilichozaa Amei na hata Lolela wananyanyasika kwa kukatazwa kwenda kulima Amei jambo ambalo linadaiwa huenda likaibua mgogoro wa wakulima ambao ulionekana kutoweka wilayani humo

Akizungumzia hilo Mbunge wa Kiteto Emmanuel Papian alisema Serikali ilichelea kutatua mgogoro toka mwanzo baada ya kubainika baadhi ya viongozi vijiji kutumia nafasi yao kufanya maamuzi ambayo yataleta madhara kwa jamii kuomba suala hilo lifikishwe kwa Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majalia kwa utatuzi zaidi

Akijibu hoja hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Tumaini Magesa alisema utatuzi wa migogori hufuata ngazi na kumtaka Mbunge huyo kufuata njia sahihi ambapo alisema baada ya wilaya ni Mkoa hivyo hawezi kuvuka ngazi ya mkoa na kwenda Taifani 

"Naomba tutumie utaratibu wa kawaida katika kutatua migogoro yetu, hapa siwezi kwenda kwa Waziri kabla ya kufika kwa Mkuu wangu wa Mkoa kama kuna uhitaji na mimi sioni kama Amei kuna tatizo kubwa isipokuwa baadhi ya viongozi ndio wamekuwa tatizo na hasa wanasiasa

Ndaki Stephani Katibu Tawala wa wilaya ya Kiteto alishauri na kuwataka wananchi kufahamu kuwa mtu yoyote anaweza kuishi kwa kufanya kazi mahali popote ili mradi afuate sheria ya eneo husika ama kijiji katika matumizi ya ardhi

Mwisho.

Maoni