TALGWU watembelea wanachama wao Kiteto

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania  (TALGWU) Mkoa wa Manyara Dr. Marting Kongola, akizungumza na wanachama Tawi la Njoro Zahanati ya Kiperesa Wilayani Kiteto Mkoani Manyara..
Katibu wa TALGWU Mkoa wa Manyara Raymond Chimbuya akifafanua jambo mbele ya wanachama Tawi la Njoro Wilayani Kiteto Mkoani Manyara..
Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji Wilayani Kiteto Dr. Steven Agostino akifafanua jambo wakiwa kwenye ziara na viongozi wa TALGWU Mkoa wa Manyara Wilayani humo..
Tabibu Ombeni Barick wa Zahanati ya Kiperesa akiwasilisha kero zake mbele ya viongozi wa TALGWU Mkoa wa Manyara
Baadhi ya wanachama wa TALGWU katika picha ya pamoja na uongozi wa Chama chao wa Mkoa Manyara



NA, MOHAMED HAMAD
UONGOZI wa Chama cha Wafanyakazi Mkoani Manyara,TALGWU umefanya ziara ya kuwatembea wanachama wao Wilayani Kiteto katika maeneo ya kazi na kuwapa matumaini pamoja na kupokea kero na changamoto zinazowakabili

Wakizungumza na wanachama Matawini katika maeneo ya Kibaya, Dosidosi,Orgine, Matui, na Kiperesa, wanachama hao wamedai kuwa wataendelea na majukumu yao ya kazi kama walivyosaini mikataba yao na kuitaka Serikali kutimiza wajibu wao

Aidha katika ziara hiyo imeelezwa kuwa baadhi ya changamoto zilizojitokeza kwa wanachama hao ni pamoja na Serikali kutowalipa baadhi ya watumishi Stahiki zao kama vile fedha za uhamisho, fedha za masaa ya ziada, (Calls allowernce) fedha za likizo, kutopandishwa madaraja baadhi yao kwa zaidi ya miaka 7

Baadhi ya watumishi kutolipwa fedha za kujikimu baada ya kuajiriwa na mishahara,  jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya kazi na mahusiano kazini namba 6. (2004) pamoja na kanuni za utumishi wa umma

Akizungumza na wanachama hao Katibu wa TALGWU Mkoa wa Manyara Bw. Raymond Chimbuya, aliwataka wanachama hao kufahamu haki zao na kuzidai kwa maandishi tofauti na ilivyo kwa baadhi ya watumishi kudai kwa maneo

"(The Goverment always works on paper) Serikali daima hufanya kazi kwa maandishi.." Sitegemei mtumishi wa Sereikali ya Dr. John Pombe Magufuli kufanya kazi kwa maneno badala ya kufanya kazi kwa maandishi na kuweka kumbukumbu, alisema Bw. Chimbuya 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TALGWU Mkoa wa Manyara Dr. Marting Kongola aliwataka wanachama hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii na uadilifu kwa jamii kama ilivyo katika mikataba yao ya ajira

Mwisho





Maoni