DC Kiteto afunga mafunzo ya mgambo tar 20.12. 2017

Mkuu wa wilaya ya Kiteto, mkoani Manyara,Tumaini Magesa katikati ya maafande wa JW na Magereza wakiimba wimbo wa Taifa la Tanzania..
Mkuu wa wilaya ya Kiteto mkoani manyara, Tumaini Magesa, akizungumza na jeshi la akiba (mgambo) ambao hawapo pichani, alipokuwa anafunga mafunzo hayo..
Jeshi la akiba (mgambo) Kiteto wakifuatilia hotuba ya mkuu wa wilaya ya Kiteto mkoani Manyara Tumaini Magesa wakati akifunga mafunzo katika kata ya Partimbo..
Kikosi cha Jeshi la akiba (mgambo) kata ya Partimbo Kiteto wakionyesha walichojifunza mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara Tumaini Magessa..
Mashuhuda akiwepo diwani wa kata ya Kibaya Kasim Msonde wakifuatilia gwaride la mgambo wa kata ya Patimbo..
Koplo wa JW Afane Robi akitena na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Tumaini Magesa..

JESHI la akiba kata ya Partimbo wilayani Kiteto mkoani Manyara lilianza tar 24.0.2017 likiwa jumla ya 193, wanaume 160 na wanawake 33, wakiongozwa na Afande Rhobi Chacha,Sajenti Safari Munah na Michael Millel

Masomo waliojifunza ni pamoja na mbinu za kivita,ujanja wa porini, matumizi ya slaha,upigaji wa shabaha na elimu ya kubaini wahamiaji haramu ambayo itawawezesha kusaidia mamlaka husika kulinda nchi dhidi ya wahamiaji

Pia katika mafunzo hayo kikosi hicho kimeahidi kutoa ushirikiano wa ulinzi pamoja na kusaidia kuondoa tatizo la mgogoro kati ya wakulima na wafugaji ambapo Kiteto iliathiriwa siku za hapo nyuma

Kwa upande wake mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kiteto Tumaini Magesa akizungumza na kikosi hicho aliwapongeza kwa kuwa wazalendo na kuwataka watimize malengo yao hasa kuilinda Kiteto na Tanzania kwa ujumla

alisema nafasi waliyoipata ni njema na inatambuliwa kisheria hivyo kuna kila haja ya kujivunia kuwa wamepitia hatua flani ambayo inafursa ya kulilinda Taifa ndani na nje ya mipaka yake kama lilivyokusudiwa

Mwisho..



Maoni