Nyumba ya mmoja wa wakazi Kijiji cha Lerug kata ya Kijungu Kiteto ManyaraTanzania..
Choo cha mmoja ya familia ya Kijiji cha Lerug kata ya Kijungu Kiteto Manyara Tanzania ambacho hutumika kwa matumizi ya kila siku..
DC Kiteto Tumaini Magesa akitoa maelekezo kijiji cha Lerug kuhusu ujenzi wa shule ya msingi..DC Kiteto Tumaini Magesa akionyesha mfano wa kujenga msingi kuwaunga mkono wananchi ujenzi wa shule ya msingi Lerug Kijungu..
Fundi wa ujenzi wa jengo la shule Lerug akiongea na mkuu wa Wilaya ya Kiteto Tumaini Magesa..
Baadhi ya wananchi akiwepo Mandalo Abilahi Diwani wakifuatilia ziara ya mkuu wa wilaya Kiteto Kijiji cha Lerug Kijungu..
Makazi ya wananchi wa Kijiji cha Lerug kata ya Kijungu, haya hapa ambapo Serikali Kiteto imewataka wabadilishe..
Mlima wa Ngapapa..wenyeji wa maeneo haya ni AKIE (wandorobo) wilaya ya Kiteto Manyara Tanzania..
NA MOHAMED HAMAD
MKUU wa wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Tumaini Magessa amewataka wananchi wa vijiji vya Lerug na Ngapapa ambao wenyeji wake ni AKIE (wandorobo) kuwa na makazi ya kudumu.
Hatua hiyo imetokana na ziara aliyoifanya na kujionea hali iliyopo kijijini hapo ambapo kwa mujibu wa taarifa za uhakika ni kwamba vijiji vya Lerug na Ngapapa wilayani Kiteto Manyara Tanzania havijawahi kupata huduma za kijamii toka miaka 24 iliyopita
Alisema wenyeji wa vijiji hivyo ni wandorobo walikuwa na tabia za kuhamahama kutafuta vyakula aina ya mizizi,asali na nyama, hivyo Serikali kwa kuthamni utu wao wakawataka waishi eneo moja ili waweze kupatiwa huduma za kijamii
Hata hivyo toka kipindi chote hicho vijiji hivyo hawajawahi kupata huduma yoyote ambapo sasa Serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Kiteto Tumaini Magessa ameamua kunusuru hali hyo kwa kuanzisha mpango wa ujenzi wa shule za msingi katika vijiji hivyo.
Kwa sasa kijiji cha Ngapapa kimefanikiwa kufikisha lenta ujenzi wa madarasa mawili huku mengine mawili yakiwa yameezekwa bati na Kijiji cha Lerug wako katika hatua ya msingi wakitaka kuondokana na adha ya kukosa elimu kwa watoto wao
Ujenzi wa shule hizo umetakiwa kuendana sambamba na makazi ya kudumu ya wananchi hao ambapo wametakiwa kujenga nyuma bora na imara ili Serikali nayo iweze kusogeza huduma karibu na wananchi hao
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni