Kiteto waungana siku 16 za kupinga ukatili..

Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi mjini Kibaya, Kiteto Manyara Tanzania wakiwa na mabango ya kupinga ukatili..
Mgeni rasmi Bi. Beatrice Rumbeli akihutubia kwenye kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia nchini ambapo kiwila zilifanyika mjini Kibaya, Kiteto Manyara, Tanzania..
Bw. Joseph Mwaleba, afisa maendeleo ya jamii Kiteto akifafanua jambo kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia mjini Kibaya, Kiteto Mnayara Tanzania..
Bi. Jackline Barongo akipeana mkono na afisa mtendaji kata Mwakibeth mara baada ya kusoma risala kwa mgeni rasmi Bi Beatrice Rumbeli mwenye gauni ya kitengo..
Maafisa maendeleo ya jamii, Bw. Rodrck Kidenya kulia na mwenzake wakifuatilia hutuba ya siku 16 ya kupinga ukatili mjini Kibaya Kiteto Manyara Tanzania..
Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi na sekondari mjini Kibaya wakifuatilia hotuba kwa mgeni rasmi ya siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia mjini Kibaya Kiteto Manyara Tanzania..


NA MOHAMED HAMAD
MKOA wa Manyara umetajwa kuongoza kwa vitendo vya ukatili hapa nchini na kuleta madhara kwa jamii hali inayosukuma Serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuingilia kati kwa kutoa elimu ya kukabiliana na vitendo hivyo.

Kufuatilia hali hiyo Serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali wameungana pamoja siku 16 za kupinga ukatili ambapo kilele chake imefanyikia mjini Kibaya Kiteto kwa kutolewa kauli ya wananchi kutakiwa kuacha tabia za ukatili.

Akizungumza na wananchi mjini Kibaya Beatrice Rumbeli ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maazimisho hayo alitaja aina za ukatili kuwa ni vipigo, ukeketaji, ulawiti, kunyimwa haki, unyanyapaa, mimba za utotoni pamoja na mfume dume uliokithiri ndani ya familia.

Alisema umefika wakati wa kupinga mila potofu na kandamizi zilizoweka mizizi ndani ya jamii na kudai kuwa kuna sheria zilizowekwa ambazo mtu akibainika mahakamani kutenda kosa hilo atapewa adhabu kulingana na kosa hilo.

Kwa upande wake Jackline Barongo afisa ustawi wa jamii katika akizungumza mbele ya wananchi hao alisema vitendo vya ukatili vinazidi kujitokeza kutokana na jamii kuviendekeza na hata vinaporipotiwa baadhi ya wazazi huchangia.

"Kesi nyingi za ubakaji na kulawiti zilizoripotiwa kiteto tumeshindwa mahakamani kutokana na jamii kuungana na watuhumiwa kwa kuhongwa ili kuharibu ushahidi ili wasipatikane na makosa jambo ambalo linatuwia vigumu kupambana nalo"

Alisema zaidi ya watoto 160 wamekatisha masomo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo mimba, utoro, ajira kwa watoto wadogo, na hata wazazi kuhamahama na watoto wao kwenda katika maeneo ambako hayana shule na kuwanyima haki yao ya elimu.

Joesph Mwaleba afisa maendeleo ya jamii Kiteto, aliwahakikishia wananchi hao kuwa Serikali itawachukulia hatua wazazi na walezi wanaoendekeza ukatili kwa watoto kuwa kufanya hivyo ni kuunda Taifa la watu watukutu.

MWISHO.

Maoni