Ujenzi wa shule vijiji vya Lerug na Ngapapa Kiteto waanza

Mkuu wa wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Tumaini Magessa akianzisha ujenzi wa shule mpya ya msingi kijiji cha Lerug kata ya Kijungu ambacho kilinzishwa mwaka 1993..
Mkuu wa wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Tumaini Magesa akitoa maelekezo ya Serikali kuhusu ujenzi wa shule mpya ya msingi Lerugu iliyopo kata ya Kijungu..
Jengo jipya la shule ya msingi Lerug kata ya Kijungu Kiteto Manyara..
Ujenzi wa shule ya msingi Ngapapa kata ya Kijungu..
Mandaro Abdilah diwani wa kata ya Kijungu akizungumzia jengo la shule ya msingi Lerug..
Serikali lazima ihakikishe kuwa inashirikiana na wananchi katika ujenzi wa shule
Kaimu Mwenyeki wa Kijiji cha Lerug akifafanua jambo..
Mkuu wa wilaya ya Kiteto akitaka ufafanuzi kwa kamati ya ujenzi wa shule ya msingi Lerug
Fundi wa ujenzi wa shule ya msingi Lerug akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Tumaini Magessa..
Kikao cha Mkuu wa wilaya ya Kiteto na wananchi wa Kijiji cha Ngapapa akiwahamasisha ujenzi wa shule ya msigi..
Wananchi wa Ngapapa wakifuatilia kikao cha harambee ya ujenzi wa shule ya msingi Kijijini kwao
Wananchi wa Kijiji cha Ngapapa wakifuatilia kikao..
Makazi ya kudumu ya mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Lerug Kiteto Manyara Tanzania
Moja ya choo kinachotumia na moja ya familia ya mkazi wa kijiji cha Lerug..Kiteto Manyara Tamzania


NA MOHAMED HAMAD
VIJIJI vya Lerug na Ngapapa vilivyopo kata ya Kijungu Wilayani Kiteto mkoani Manyara, havina huduma za jamii kama vile shule ya msingi, maji, zahanati na hata barabara toka vianzishwe miaka mingi iliyopita.

Kijiji cha Lerug kilinzishwa mwaka 1993 kikiwa na idadi ya wananchi inayokidhi kuanzishwa kwake kwa lengo la kuwapatia wananchi huduma za jamii karibu, lakini hadi 2017 hakuna huduma iliyowafikia na kusababisha adha kubwa kwa wananchi hao.

Kipindi chote kumekuwepo na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na hata Serikali wakijaribu kuwasaidia kupata huduma hizo lakini hawajafanikiwa kupata hivyo kuwafanya wananchi hao kulalamika kila kukicha.

Kutokana na hali hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Tumaini Magessa katika ziara zake aliambiwa hitaji la wananchi hao ambao kwa sasa ameamua kuanzisha ujenzi wa shule ya msingi na baadaye zahanai pamoja na maji.

Wananchi hao wameridhia ushauri huo ambapo kila kijiji kimeanzisha ujenzi wa shule huku Serikali ikiwa mstari wa mbeli kuchangia ili waweze kupata huduma ya kwanza ya elimu kisha zingine zifuate.

 Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kiteto ilitoa fedha katika kila kijiji laki tano na sasa imeongeza zingine huku mbunge wa Jimbo la Kiteto Emmanuel Papian akitumia mfuko wa Jimbo kwa kuwapa mil 1 kila kijiji pamoja na fedha za ziada laki mbili.

Akizungumza na wananchi hao ambao kwa sasa wamelalamika kuwa wanalazimika kuishi katika makazi ya muda kutokana na wenyeji wa kijiji hicho kabila la (AKIE) kukataa kujengwa nyumba za kudumu, aliwataka kila mmoja atumie fursa ya kuwa hapo kujenga nyumba za kudumu.

" Jengeni nyumba za kudumu..haiwezekana unakuja kijijini huwezi kupata hata kiberiti, awali nilianza kufikiria kutaka kuvunja kijiji hiki lakini hapana.. naagiza ili mpate nusura jengeni nyumba za kudumu muweze kupata huduma za jamii Kijijini"

Hizi nyumba zenu ni kama mmekuja kwa muda ili baadaye muondoke..sasa serikali hatutaki kuona hali hiyo tunataka muwe na makazi ya kudumu ili hata tukileta miradi ije kuwa salama hapa Kijjini.

Hatua hiyo imetokana na malalamiko ya wananchi kuwa kumekuwepo na ukabila kijijini hapo kuwa wenyeni hawataki kuwapa viwanja vya kujenga makazi ya kudumu wageni, kwa madai kuwa watanufaika na ardhi yao.

Baada ya kufuatilia imebainika kuwa baadhi ya wanajamii ya kifugaji maasai wamekuwa na kauli kwa kabila hilo la AKIE kuwanyima fursa mbalimbali makabila mengine kama vile ardhi na hata mazao ya misitu

Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya ya Kiteto aliwaambia waanchi hao kuwa wafuate taratibu za kisheria ili waweze kupatiwa haki ilimradi kuwa ni raia wa Tanzania ambao wana haki ya kuishi popote ilimradi wasivunje sheria..

Mwisho

Maoni