Tamimu Kambona (DED) Kiteto akiongea katika moja ya kikao ..
NA. MOHAMED HAMAD.
NIMPONGEZE Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya
wilaya ya Kiteto, Tamimu Kambona, kwa kuonyesha uwezo wa kiutendaji, katika
kusimamia miradi ya maendeleo sambamba na kupunguza mang’unguniko ya wananchi.
Hali hiyo imewapa wananchi matumaini makubwa kwa
mkurugenzi huyo, hasa alipoweka kambi vijiji vya Sunya na Kijungu kusimamia
miradi ya ujenzi kwa lengo la kufikia malengo tarajiwa.
Kambona aliteuliwe miezi 18 iliyopita kushika
wadhifa huo baada ya kuteuliwa na Rais Dr John Magufuli, akitokea Mtwara kama
afisa elimu,na Wilaya Kiteto ni ya
kwanza kuhudumu katika wazifa huo.
Kiteto ilionekana eneo la wapiga dili kwa baadhi ya
watumishi wa Serikali hasa katika usimamizi wa miradi ya maendeleo, hali
iliyofanya wananchi kutowaamini viongozi wao huku wakiomba Serikali kuwabadilishiwa
viongozi.
Kambona alianza kusimamia miradi ya ujenzi, ambapo
awali ilionekana maeneo mengine yakilalamikiwa na wananchi kwa kujengwa chini
ya kiwango huku kukiwa hakuna hatua dhidi ya wasimamizi hao.
Miongoni mwa majengo bora yaliyompa sifa mkurugenzi huyo
ni ujenzi wa nyumba moja ya walimu inayotumiwa na familia sita kata ya Sunya ya
thamani ya mil 150, madarasa nane Vijiji vya Kijungu na Sunya pamoja na matundu
24 ya vyoo katika vijiji hivyo.
Kambona amesimamia ujenzi wa uzio wa hospitali ya wilaya
ya Kiteto wa thamani ya mil 37, pamoja na ukarabati wa soko la wilaya, ambalo
awali liliungua moto kwa zaidi ya miaka minne iliyopita 2015.
Halmashauri ya wilaya inauwezo kuhudumia wananchi
wake maji safi na salama kwa 36% ya sasa ambapo kwa jitihada sa zaza za
kuchimbwa visima 21 katika maeneo mbalimbali kuongeza kiwano na kufikia 50% ifikapo
mwezi wa tatu mwaka huu.
Hatua iliyofikiwa katika jitihada hizo ni
kutengeneza miundombinu ya maji ambapo wakandarasi wanaendelea na usanifu huku
msimamizi mkuu akiwa mkurugenzi huyo ambao hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa
Manyara Alexander Mnyeti alimpa sifa kwa utendaji wake wa kazi
Wilaya ya Kiteto haikuwa na shule ya kidato cha sita
hivyo Kambona kwa kushirikiana na wananchi hao amefanikiwa kuanzisha shule
Mbili za Kiteto Sekondari na Engusero na sasa zimeanza kupokea wanafunzi kutoka
maeneo mbalimbali hapa nchini
Waziri wa Tawala na Serikali za mitaa, Seleman Jafo,
mwezi mmoja uliopota akiwa Kiteto alitembelea Sekondari ya Enguseri na kujionea
jitihada hizo na kuahidi kuipa shule
hiyo fedha kwaajili ya ujenzi wa mabweni ambapo kwa mujibu wa Kambona alikiri
kupokea fedha hizo.
Jitihada hizo Serikali imetoa mil 400 zingine kwaajili
ya uboreshaji wa kituo cha afya Sunya ambapo kazi ya ujenzi imeanza kwa lengo
la kupunguza manung’uniko ya wananchi katika huduma ya afya.
Ujenzi wa mitaro wa zaidi ya mil 100 mjini Kibaya umekamilika,
huku Sekondari ya kata ya Partimbo ukikamilika na kutakiwa kuanza kupokea
wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018
Kimsingi waswahili wanasema mnyonge mnyongeni haki
yake mpeni..kauli hii naiunga mkono na hasa nikipongeza Serikali kwa kuonyesha
imani kwa mkurugenzi huyo kwa kutoa fedha nyingi katika miradi ya maendeleo ya
wananchi Kiteto.
Mwisho.
Maoni
Chapisha Maoni