Naibu Waziri Stanslaus Nyongo Angalia Moja Ya Mashimo Ya
Uchimbaji Madini Ya Dhahabu..
Wachimbaji wadogo walijitokeza kumskiliza Naibu waziri..
Wachimbaji wadogo walijitokeza kumskiliza Naibu waziri..
WAZIRI wa madini, Stanslaus Nyongo, amewata wachimbaji wadogo wa
mgodi wa Nyakafulu uliopo wilayani Mbogwe mkoani Geita kudumisha amani
na utulivu pamoja na usafi wa mazingira ili kuepukana na magojwa ya mlipuko.
Alisema iwapo kukatokae magonjwa ya mlipuko
kama kipindupindu, mgodi huo utafungwa ili kunusuru maisha ya
wananchi kutokana na kushindwa kwao kuzingatia usafi katika maeneo hayo ya
mgodi.
Hata hivyo aliwataka wachimbaji hao kuzigatia sheria na taratibu
za nchi akisema kila mtu achimbe kwa kuzingatia taratibu na sheria kwani hakuna
mwenye leseni ya eneo hilo, hivyo haitaji kusikia mtu akinyanyaswa wala
kudhulumiwa.
“Mpo hapa kwasababu ya kauli ya Mh. Rais wa Jamuhuri ya
muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Makufuli, lakini vilevile akisikia kwamba
hapa hakuna amani na sio wasafi mimi nitatoa amri ya
kufunga mgodi huu kwani wizara yangu ndio inahusika kutoa leseni
hivyo pamoja na hayo yote amani itawale”alisema Naibu waziri.
Aidha aliwakumbusha kulipa kodi ili waweze kuchimba
kwa kufata taratibu, sheria, na kanuni za nchi bila kubugudhiwa na
mtu yoyote na wangawane kwa utaratibu bila kudhulumiana kwa sababu sehemu
wanayochimba kuna leseni ya mtu kwaiyo wachimbe kwa kuweka akiba ili na wao
baadae wakate leseni zao za uchimbaji.
‘’Wachimbaji mmekuwa na tabia ya kula bata na kuhonga pesa zote
mnapouza madini acheni tabia hiyo wekeni akiba mkate leseni zenu za
uchimbaji, ili muweze kutambulika kisheria” alisema Waziri
Pia aliunda kamati itakayokuwa chini ya mkuu wa wilaya ya
Buselesele, ambayo itasimamia suala la kugawana asilimia ambapo
kwa upande wa wasimamizi wa mgodi huo Isanja badugu watakuwa wawili watu wawili
kutoka kwa wachimbaji na watu wengine wawili kutoka kwa wenye mashamba
wachanguane wapange namna ya kugawana asilimia kwa amani.
Aidha wachimbaji hao walimuomba Naibu waziri wa madini
kuwasaidia kupata leseni ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira yao na vitendea
kazi kwasababu wamekuwa wakitumia njia za asili katika kufanya shughuli zao za
uchimbaji.
Machimbo hayo Nyakafu ambayo yanakadiliwa kuwa na
wachimbaji elfu mbili kutoka sehemu mbalimbali ambapo swala usafi wa limekuwa
ni changamoto kwa kukosekana vyoo na maji safi.
MWISHO.
Maoni
Chapisha Maoni