Babati kutatua changamoto zinazowakabili wajasiriamali

Serikali Wilayani Babati imepanga Kutatua changamoto wanazokabiliana nazo Wanawake wajasiliamali katika kukuza shughuli zao za ujasiliamali na kujiongezea kipato.

Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Eng Raymond Mushi ambaye alikuwa Mgeni Rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Kiwilaya Tarafa ya Mbugwe kata ya Mwada.

Kabla ya Hotuba , Mgeni Rasmi amekagua Kazi /shughuli wanazofanya wanawake na kuwapongeza kwa kuendeleza shughuli za ujasiliamali na kukuza viwanda. Aidha Mgeni Rasmi ameongoza Wananchi kupima Afya zao.

Maoni