CHAMA cha mapinduzi, CCM wilayani Kiteto mkoani Manyara kimesema, kimeridhishwa na utekelezaji wa Ilani yake unaofanywa na Serikali.
Katibu wa CCM Kiteto, Eng Pashue Shekue alisema, kazi inayofanywa na Mkurugenzi Kambona ni zaidi ya walichofikiri
" Tuendelee kumpa nafasi Kambona kufanya kazi aliyoagizwa na mwajiri wake sisi kama chama hatuna maneno naye hata kidogo"
Alisema wananchi wanataka kutika kwa viongozi ni huduma za jamii, tena bila mashart, hivyo kinachotakiwa ndicho kilichopo
Katika ukaguzi wa miradi uliofanywa na kamati ya siasa ya Wilaya akiwemo mkuu wa Wilaya ya Kiteto Tumaini Magesa, walipitia miradi ya Elimu na Kilimo
Tumejionea Majengo mengi yaliyojengwa kwa Fedha kidogo na bora ambayo, hakuna Mwananchi aliyethubutu kuhoji dhidi ya kupongeza
Kilimo napo tumeona, ila ushauri abane maafisa kilimo zaidi waweze kusaidia wananchi kuondokana na kilimo cha mazoea
Utakuta mkulima analima ekari 100 anapata gunia 50, hali kadhalika mifugo mingi isiyo na tija, chama tunataka Idara hizi mbili zifanye kazi ya wananchi matatizo ya Kiteto yatakwisha
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kiteto na mjumbe wa kamati ya Siasa alisema, atahakikisha anasimamia sheria kikamilifu ili ila Mwananchi apate .anufaa
Wapo baadhi ya wananchi wanaolalamika, nisema lazima tuwarejeshe katika sheria kwani awali waliishi kwa mazoea
Hii ni Serikali ya awamu ya tano ambayo inataka kuona matokeo, sitaki nije kuondoka wasinikumbuke wananchi, lazima niache alama, alisema Magesa
Kwa upande wake Mohamed Kiyondo MKT wa CCM Kiteto alisema, Kiteto ilichelewa miaka mitano kwa kugombea ardhi huku huduma zingine zikizorota
Mwisho.
Maoni
Chapisha Maoni