DC Kiteto ashauri vikundi kuanzisha viwanda

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, mkoani Manyara, mhandisi Tumaini Magesa, amevitaka vikundi kuanzisha viwanda, kuunga mkono jitihada za Serikali.

Wilaya ya Kiteto, imetakiwa kuwa na viwanda 15, katika mkakati wa mkoa ambapo wadau mbalimbali wameaswa kuunga mkoni.

Akizungumza na wanachama hao, ambao asilimia 100 ni wanawake, mkuu huyo wa Wilaya akisema, wanawake wananafasi  kubwa katika maendeleo.

"Ninyi pamoja na utengenezaji wa batiki, na bidhaa zingine mbalimbali, kuweni na mtaji wa tsh mil 3 nitaongeza ili mnunue mashine"

Najua hamuwezi kosa, kwani hata ninyi wenyewe mnauwezo mkubwa, kusaidiana nawapeni wiki mbili kukamilisha zoezi hilo

Kaimu mwenyekiti wa kikundi hicho, mama Kalwan alimwomba mkuu Huyo wa Wilaya kuhakikisha wanapata ofisi pamoja na vitendea kazi kutokana na wao kuwa tayari kushirikiana na Serikali

Katika ombi hilo, Magesa aliwahakikishia wanachama hao kuwa watafanikiwa kupata eneo kwaajili ya kujenga ofisi kupitia Idara ya ardhi

Mwisho

Mwisho

Maoni