Ilikuwa ni ziara ya Kikazi kata ya Bendera Wilaya ya Same.kama ilivyo desturi ya DC wa Same kila jumatatu na Alhamisi kuwa ni siku za kuenda kwa wananchi.
🔸Ashirikiana Na wananchi kusafisha Barabara.
🔸Akaa Na Viongozi ( WDC ) Na kuwaasa kutowachelewesha wananchi kwenye maendeleo.
🔸Asikiliza kero za wananchi - mkutano
wa hadhara Na kutoka mujibu ya kero
🔸 Aagiza wataalamu kumpa majawabu ndani ya wiki mbili Juu ya kero kubwa ya mgawanyo wa Maji ya umwagiliaji.
🔸Awakumbusha wananchi kushika leseni za madini Na kuanza kuchimba Gypsum. Kwani ina ubora kuliko maeneo mengi.
🔸Aagiza Kijiji kutenga eneo lenye madini hayo kwa ajili ya vijana.
🔸Aahidi kuwaagiza idara ya madini kuja kuwapa elimu wananchi Juu ya taratibu za kupata leseni Na uchimbaji.
🔳Atembelea shule Na kukutana Na tatizo la wanafunzi kubakwa.
🔳Akasirishwa Na kuondoka Na muhusika. Na watoto wanne wa kike walihohusika.
🔳Aagiza Polisi kufungua kesi haraka. Aagiza mashahidi kutoa ushirikiano.
Mkuu huyo wa Wilaya Mh. Rosemary Senyamule aliongozana Na wataalamu toka halmashauri Tar. 12/03/2018
Maoni
Chapisha Maoni