Wakulima wilayani Kiteto mkoani Manyara, wanakusudiwa kuanza kutumia teknolojia za kisasa za kupalilia mazao shambani.
Akizungumza na baadhi ya wakulima wakati wa jaribio la kupalilia kwa kutumia teknolojia ya kisasa, mkuu wa Wilaya Mhandisi Tumaini Magesa alisema, wakulima watanufaika na mpango huo.
Alisema wakulima wanatumia muda mwingi pamoja na fedha kuajiri vibarua wa kupalilia mashamba yao, na sasa wataanza kunufaika kwa kuwa na mtambo wa kupalilia
Najua mtakapoanza kutumia zana hizi mtapata hata muda wa kufanya shughuli zingine za kiuchumi, badala ya kuwa na kilimo miaka nenda rudi, alisema Magesa
Kwa upande wake mkulima Ntomolla Ntomolla alisema, Fedha nyingi za wakulima zinaishia kuajiri vibarua na kuwagharimikia mahitaji mbalimbali
"Hapa utawanunulia chakula, mavazi na hata madawa kwakuwa uko nao, ila ni gharama na wakati mwingine wanatoroka shambani" alisema.
Machine hii nadhani itasaidia kwani tumeambiwa humu kuwa inauwezo la kulima mpaka ekari tatu kwa Siku mtu mmoja, wakati kwa jembe la mkono hata nusu eka mtu hafikishi
Kwa mujibu wa mkuu wa Wilaya alisema machine hiyo iko katika majaribio na amebaini kuwa jitihada za mtu ndizo zitaongeza ukubwa wa eneo lake katika palizi.
Mwisho.
Maoni
Chapisha Maoni