Viongozi Kiteto ondoeni tofauti zenu..

                                              Naibu Waziri TAMISEMI, Joseph Kakunda..


Na MOHAMED HAMAD
Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, imekuwa na changamoto ya ya kisiasa inaendelea kuwagharimu wananchi.

Kila kiongozi anayefika, lazima agusie na kuwasihi viongozi kuacha siasa na badala yake wawatumikie wananchi

Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa, alikuwa wa kwanza kuwaambia viongozi hao kuacha siasa na kuwatumikia wananchi

Majaliwa alifika Kiteto kusuluhisha wakukima na wafugaji, ambao walihasimiana na kusababisha madhara yakiwemo maafa

Pia Waziri Selemani Jafo wa TAMISEMI baada ya kuitembekea wilaya hiyo aliwasihi viongozi hao kutanguliza maslahi ya umma mbele

Hali kadhalika Naibu Waziri wa Tamisemi Joseph Kakunda naye alipofika Kiteto alikutana na mvutano wa kisiasa ambao unazidi kutishia amani ya wananchi

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti, katika ziara yake ya siku saba wilayani Kiteto, aliwaonya wanasiasa hao  akisema yeye sio mkuu wa MKOA wa maboksi hivyo atashuhulika nao

Viongozi waliotajwa kuvutana kisiasa ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya, Lairumbe Mollel (CCM) na Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Emmanuel Papian (CCM)

Kwa mujibu wa viongozi hao imeelezwa kuwa wanasiasa hao tena wanaotokana na Chama cha mapinduzi CCM wamegawa wananchi

Mmoja amedaiwa kuwa upande wa wakulima na mwingine wafugaji, hivyo hali hiyo kusababisha mvutano mkubwa ndani ya jamii

Maagizo yanayotolewa na Serikali wakati mwingine hupigwa na makundi hayo kutoka na na mgawanyo huo

Lairumbe Mollel mkt wa hlm ya Kiteto alisema kama ana tatizo lililosababisha ngogoro yuko tayari kukamatwa na kwenda kuhojiwa popote

Naye Mbunge wa Kiteto Emmanuel Pipian akizungumzia hayo alisema hana ubaguzi kwa wananchi wa Kiteto kati ya mkulima na mfugaji wote ni wake

Kwa muda mwingi sasa wananchi wa Kiteto wamekuwa hawapati huduma za jamii kwa kiwango stahili kutokana na viongozi kushughulikia migigoro ya ardhi kuliko shughuli zingine za maendeleo

"Nimechoshwa na migogoro..kila ukiamka kutaka kufanya shughuli zenye tija kwa umma kama afya, elimu, maji na hata barabara, unabaki kushugulikia migogoro ya wakukilima na wafugaji" alisema Tamimu Kambona Mkurugenzi wa halm ya Kiteto

Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, Tumaini Magesa, alisema hajaja kutengua Torati  na badala yake atasimamia kile kilichopangwa na vijiji kisheria

"Sijaja kutengua Torati..hapa ninachosimamia ni maamuzi yenu mliyoamua wananchi huko vijijini..na hii ndio kazi ya Serikali" alisema Magesa.

Maoni