Kifo cha Victor Kimesera kimegusa nyoyo za wanakiteto kufuatia ushiriki wake katika masuala ya kijamii hasa siasa
Marehemu Kimesera ambaye pia alijuwa ni makamu mwenyekiti wa Chadema Taifa ineelezwa pengo lake halitozibika.
Alikuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya Chadema Jimbo la Kiteto bila mafanikio na alishiriki shughuli za maendeleo wilayani humo.
Kwa Kipindi chote aliweza kufika Kiteto mara kadhaa akitokea Dar kuona wazazi wake pamoja na ndugu na marafiki
Baadha ya wananchi walisema, watamkumbuka Kimesera kama mmoja wa wapambanaji wa maendeleo Kiteto.
Pia Kimesera katika mchango wake aliweza kujenga maktaba yenye hadhi ya Kitaifa chini ya ufadhili wa rafiki zake watu wa Marekani.
Maktaba hiyo ilifunguliwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Ngoyai Lowasa
Aliwezesha shule pekee ya Sekondari Kiteto wakati huo vitabu na walimu wa masomo ya sayansi kutoka Marekani kama mchango wake wa kielimu.
Akiwa Kiteto katika mikutano yake aliwataka wananchi kujiendeleza kuwa wabunifu na kudai haki.
Kwa mujibu wa Bakari Soka Katibu wa Chadema wilaya alisema kifo cha Kimesera kimeacha pengo kubwa kisiasa Kiteto na hapa nchini
Alisema alikuwa ni mwanzilishi wa Chadema akiwa na akina marehemu Edwine Mtei na wengine mwaka 1992
Hakuwa MTU wa majivuno asiyekubali kushindwa kwani wakati wote alionekana mcheshi kwa wafuasi wa vyama vyote
Mungu ametwaa, Mungu ametoa jina la Mungu lihimidiwe..kauli za baadhi ya waliopata taarifa za msiba huo Kiteto
Maoni
Chapisha Maoni