NGO ya VOEWOF yadhamiria kuimarisha matumizi ya nishati mbadala Wilayani Same..
Katika kikao kilichofanyika Tar 20/03/2018. Wadau wa mazingira walieleza sababu zinazopelekea watu kutochangamkia nishati mbadala pamoja na juhudi za serikali na wadau kuhimiza matumizi yake.
Baadhi ya sababu zinazotajwa ni:-
đź’ˇKutopatikana nishati hiyo vijiji Mf. gas
đź’ˇGharama kubwa ya nishati mbadala, pia kodi katika bidhaa hizo.
đź’ˇMazoea na utamaduni
Ambapo nishati ya kutumia Mkaa na kuni vinapelekea uharibifu mkubwa wa mazingira na upungufu wa maji.
đź’ˇWadau wakubaliana kuongeza matumizi, kubuni na kuanzisha nishati mbadala yenye gharama nafuu,
đź’ˇkuendelea kuelimisha juu ya athari ya mazingira na uwepo wa nishati mbadala.
đź’ˇKuhimiza matumizi ya "interlocking block" badala ya tofari za kuchoma.
đź’ˇKusimamia sheria.
đź’ˇShirika la VOEWOF linalofanya kazi chini ya CARE International linafanya kazi na vikundi vya wanawake.
đź’ˇlimewezesha majiko ya gas zaidi ya 300 kutumika vijijini.
đź’ˇLimepania kuanzisha viwanda vya kutengeneza nishati mbadala kwa kutumia taka.
đź’ˇWilaya yaahidi kutoa eneo, kutoa mikopo kwa vikundi hivyo na kutumia miti inayooteshwa na vikundi hivyo.
Kikao hicho pia kimewashirikisha DC wa Same, wataalamu toka ofisi ya RC Kilimanjaro na halmashauri ya Same, TBS, wanazuoni toka SUA, TRA, wauzaji wa nishati mbadala, wanavikundi hao na vyombo vya habari.
DC Same alipongeza na kuwashukuru VOEWOF Na wadau wengine jinsi wanavyoshiriki kuibadilisha Same, kila mmoja kwenye nyanja yake. Alikiri kuwa kwa kasi hii; Wilaya ya Same itafikia malengo yake ya kubadili mazingira ya Same.
" Same is not same"
Maoni
Chapisha Maoni