Bil 5 zatumika kujenga ukuta Mirerani

Manyara Tanzania..

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Meja Jenerali Martin Busungu amesema, gharama za ujenzi wa ukuta wa mgodi wa Tanzanite,  ni Sh5 bilioni.

Jenerali Busungu amesema kuwa ukuta huo wenye kilometa 24.4 utazunguka eneo lote la mgodi wa Tanzanite na tathmini ya awali, ilionyesha kwa kilometa 21 zingetumika Sh 4 bilioni.

Akizungumza Aprili 6 katika uzinduzi wa ukuta huo, Busungu amesema vikosi 20 vya JKT vimejenga ukuta huo.

“Tumetekeleza kwa uadilifu na uamnifu ujenzi huu. Tunatoa shukran za dhati kwa taasisi za uhandisi Tanzania kwa ushirikiano wao,” amesema

Amesema Jeshi la JKT lipo tayari kutekeleza maaagizo yoyote yakatayotolewa kwa mustakabali  wa Taifa.

“Kulikuwa na changamoto ikiwamo ugumu wa ujenzi hasa katika miamba, uwepo njia za nyingi za maji ambazo hata hivyo wahandisi wa Pangani River walisaidia,” amesema

Kwa hisani ya (Mwandamizi) Jeseph

Maoni