DC Kiteto afanya ukaguzi kituo cha Afya Sunya

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhandisi Tumaini Magesa, amefanya ukaguzi mradi wa kituo cha Afya Sunya na kutoa maelekeza ya Serikali kwa mafundi kujenga kwa ubora unaotakiwa.

Ameyasema hayo kufuatia kauli ya Serikali kutaka miradi ya maendeleo ya wanananchi kukagukiwa kila mara ili ilete tija.

Akizungunza na baadhi ya wananchi wa Sunya, Mhandisi Magesa alisema, nia ya Serikali ni kuona wananchi wakinufaika na miradi yao.

Katika hatua hiyo alitaka kuungwa mkono jitihada za Mkurugenzi mtendaji wa halm ya wilaya Tamim Kambona za kuwa  muadilifu katika miradi ya wanananchi

Alisema Mkurugenzi amekuwa mstari wa mbele kusimamia kwa nguvu zake zote miradi hiyo akisema, wananchi wananafasi kubwa kuifanya miradi yao kuwa endelevu.

Kwa upande wake Mzee Puputo akizungumza mbele ya Mkuu huyo wa Wilaya alisema, uboreshaji wa kituo cha Afya Sunya ni historia Kijijini hapo.

"Tunamshukuru Mkurugenzi wa Kiteto kwa jitihada zake, nasi wananchi tutakuwa makini kuulinda mradi huu ili ulete tija kwetu"

Naye katibu wa msitu wa mbao wa asili SULEDO, Bw. Msimbazi alimwahidi Mkuu huyo wa wilaya kuwa uongozi wa msitu huo umekubali kuchana mbao za mninga kwaajili  ya milango ya kituo hicho

"Tumepokea maombi ya wenzetu kamati ya ujenzi, tutawapa mbao aina ya mninga..na huu ni mchango wetu katika ujenzi huu" alisema Msimbazi

Mwisho

Maoni