Mkuu wa wilaya ya mbulu Chelestino S Mofuga leo 2/4/2018 amefunga mashindano ya bonanza la pasaka ambapo timu zilizoshindana ni matipa na sinde na ambapo matipa wamepata magoli 2 kwa 1.
Akiongea wakati wa kufunga bonanza la pasaka mkuu wa wilaya amempongeza Mh mbunge wa mbulu mjini kwa kudhamini mashindano hayo.
Pia amempongeza mh mbunge Zacharia Peter Isaay kwa kazi nzuri anazofanya jimboni mwake katika kuwaletea wanançhi maendeleo, ametaja baadhi ya fedha zilizoletwa na serikali ya awamu ya tano kuwa ni bilioni 13, ambazo zimetengwa kujenga daraja la magara, kuwa barabara ya karatu -mbulu-Haydom ipo hatua ya mwisho kufanyia upembuzi yakinifu ili kujengwa kwa kiwango cha lami,
Zahati ya Daudi na Tlawi kila moja imepata milioni 500 kwa ajili ya kupanua kuwa kituo cha afya na milioni 200 kama vifaa tiba.
Mkuu wa wilaya akipongeza kazi za mbunge na serikali kwa ujumla amesema chief sarwatt sekondari ya mbulu mjini na Yaeda chini zimepata milioni 215 kila moja kutoka mfuko wa Mamlaka ya elimu TEA.
Kuhusu michezo amewaomba wadau wa mbulu kujitokeza kufadhili timu hizo ili vijana waondokane na unywaji wa gongo, ulevi, uzuraji na kukuza vipaji vyao sambamba na kujenga afya.
Maoni
Chapisha Maoni