Mkuu wa wilaya ya Mbulu chelestino s Mofuga leo 01/04/2018 ameshiriki ibada ya Pasaka katika Kanisa la Kihistoria la Sanu ambalo inasemekana ni la pili katika ukubwa barani Afrika .
Mkuu wa wilaya akitoa salamu za pasaka katika Radio Habari njema amewashauri viongozi wa dini wakristo na Waislamu kufuata na kuzingatia katiba ya Jamhuri wa Tanzania ili watanzania waenzi na kutunza tunu za Taifa letu , za Amanj, utulivu na usalama wa Raia na mali zao.
Pia amewashauri wananchi wa mbulu na Tanzania kwa ujumla kuzingatia katiba ya Jamhuri wa muungano wa Tanzania na sheria zilizopo ili kulinda Amani, utulivu na Usalama wa Taifa letu.
Pia amekemea wananchi wa mbulu kutojihusisha na kushiriki maandamano yanayohamasishwa kwenye mitandao na mtu anayejulikana kwa jina la Mange Kimambi.
Maoni
Chapisha Maoni