DC SAME AHIMIZA MSARAGAMBO

DC SAME AHIMIZA MSARAGAMBO

Ni utamaduni wa wananchi wa Wilaya ya Same kufanyakazi za jamii kila jumatatu.

Mkuu wa wilays ya Same ameungana na wananchi wilayani humo kusafisha mfereji wa umwagiliaji Kijiji cha Ruvu Mbuyuni Kata ya Mabilioni.

Pia alikagua ujenzi wa madarasa na  kusikiliza kero za wananchi ambao waliomba barabara na calvat ili waweze kusafirisha mazao yao.

Waliomba kujengewa mifereji ya maji ili  kupunguza upotevu wa maji ambapo walihimizwa kujiunga na bima ya Afya

Katika hatua hiyo waliagizwa kujenga zahanati ili kuondokana na adha ya kufuata Huduma umbali wa km. 25

Viongozi wa vijiji waliagizwa kumaliza migogoro ya Ardhi ndani ya wiki moja, na msaragambo ufanyike kwa maarifa, vifaa viwepo vya kutosha.

Vikundi 3 vilipewa mikopo ya serikali, na pia walihimizwa kukamilisha miradi kwa wakati hasa ujenzi wa maboma ili serikali imalizie palipobakia.

"Tumuunge mkono Rais wetu Mh. Dr John Pombe Joseph Magufuli anayetaka maendeleo yaende Kwa haraka, Darasa tulilokuwa tunajenga kwa mwaka mmoja, sasa tujenge kwa miezi sita"

DC Mary aliagiza kila jumatatu wataalamu washinde vijijini kuwahamasisha wananchi kwenye kazi za maendeleo, kutatua kero zao Na kukagua miradi ya idara zao.

Katika hatua hiyo mkuu huyo wa wilaya avalishwa vazi linalompa kuwa Aleigwanani wa wanawake wa kimasai.

Hatutalala mpaka Same itakapopiga hatua nyingine za maendeleo.

Maoni