Kila mwanaume anazaliwa na Tezi dume. Tezi dume siyo ugonjwa bali ni kiungo Kama viungo vingine mwilini.
Tezi dume inapatikana katika mfumo wa uzazi wa mwanaume katika shingo ya kibofu cha mkojo.
Kazi yake kubwa nikutengeneza maji maji ya uzazi wa mwanaume (shahawa), ambayo husaidia kurutubisha mbegu za kiume zilizo tengenezwa kutoka kwenye Korodani; na husaidia mbegu za kiume kubaki hai kwa muda unaostahili.
Tatizo linakuja kiungo hiki kinapoanza kutanuka. Kiungo hiki kinatanuka taratibu taratibu mnoo. Hili ni tatizo linalowakumba wanaume wengi.
Takwimu zinaonesha kwamba kati ya wanaume 10, wa 5 na kuendelea wana dalili za kutanuka kwa Tezi dume.
Ukuaji wa Tezi dume ni ile hali ya chembe chembe hai katika tezi ya kiume kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili katika eneo linalo zunguka mirija ya kupitisha mkojo na mbegu za kiume.
Tatizo hili kwa sasa linawapata wanaume kuanzia umri wa miaka 25 na kuendelea, tofauti na awali lilikuwa miaka zaidi ya 50.
Takwimu kutoka kwenye shirika la CHRP (Centre for Human Right Promotion), zinaonesha kwamba kiujumla kila mwanaume katika maisha yake ana 16% za kugundulika na saratani ya Tezi Dume, mtu 1 kati ya watu 6 analo hili tatizo; 3% (1 kati 33) wanakufa kwasababu ya Saratani ya Tezi Dume.
Saratani hii inaua mwanaume mmoja kila baada ya dakika 13.
VYANZO VINAVYOPELEKEA TEZI DUME KUTANUKA
Tatizo la kutanuka kwa tezi dume limekuwa kwa kasi sana hii ni kutokana na mitindo ya maisha wanaume wengi wanayoishi. Pia na elimu ndogo iliyoko kwenye jamii kuhusu afya zao.
Vifuatavyo ni vyanzo vya kutanuka kwa tezi dume:
- Ukosefu wa lishe kamili na Virutubisho muhimu mwilini.
- Uwepo wa sumu nyingi mwilini.
- Kutokufanya mazoezi.
- Matumizi ya pombe kali, na uvutaji wa sigara.
- Uzito mkubwa (uliopindukia, uliokithiri), na Kitambi.
- Kutokukaa sawa kwa vichocheo vya mwili (Hormone Imbalance).
- Msongo wa mawazo (Stress).
- Magonjwa ya zinaa.
- Umri mkubwa.
- Upasuaji wa korodani, kuzaliwa na korodani moja.
- Historia ya Familia (Kurithi).
- Mazingira (Ethnicity).
DALILI ZA KUTANUKA KWA TEZI DUME
Mpaka mtu apate saratani ya Tezi Dume (Prostate Cancer), ujue amekaa na tatizo hilo kwa muda mrefu, si chini ya miaka isiyopungua 10.
Hii hutokana na mrundikano wa mkojo unaobaki kwenye kibofu na kwenye mrija wa mkojo (Urethra) wakati unakojoa; ukiendelea kujirundika kwenye kibofu na mrija; baada ya muda unazalisha “Uric Acid” na ndio inatengeneza saratani (cancer).
Saratani ziko stage nne. Ya kwanza na yapili ukiwahi unaweza kupona; lakini ikishafika stage ya 3 na 4, hazitibiki. Unasaidiwa kupunguza makali kwa mionzi ukijitayarisha kupoteza maisha muda wowote.
Hivyo ukiona dalili mojawapo kati ya hizi chukua tahadhari na hatua mapema kabla hujaharibu mfumo wako mzima wa uzazi wa mwanaume.
a) Dalili za awali
- Kukojoa mkojo uliochanganyikana na damu
- Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
- Maumivu kwenye mfumo wa mkojo
- Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
- Kuhisi kibofu kimeja mkojo muda wote na ukienda kukojoa mkojo hautoki, lakini ukirudi kukaa unahisi kukojoa tena.
- Homa
- Kukojoa mara kwa mara wakati wa usiku
b) Dalili za mtu aliyeathirika
- Maumivu ya mifupa hasa chini ya mgongo, kiuno na mbavu
- Miguu kuwa dhaifu
- Kushindwa kumudu tendo la ndoa, au Kuhisi maumivu makali wakati unamaliza tendo la ndoa
- Kushindwa kuzuia mkojo, pindi unapohisi kukojoa
- Kushindwa kuzuia haja kubwa (kinyesi cha maji maji)
- Tumbo kuja gesi mara kwa mara
MADHARA YA TEZI ILIYOTANUKA
Katika hatua za awali, tezi inapotanuka hugunduliwa kwa kupimwa kwa njia ya kidole. Hii ni njia ambayo daktari huingiza kidole kwenye njia ya haja kubwa ili kuweza kubaini kama tezi imetanuka.
Kipimo hiki ndicho rahisi kinacho kubalika duniani kote na kisicho na gharama. Lakini kimekuwa kikipata upinzani kutoka kwa wanaume kutokana na imani potofu ya wahusika wa tatizo hili kuona ni udhalilishaji.
Kipimo kingine ni kipimo cha damu. Damu huchunguzwa aina ya protein inayozailishwa na seli za tezi dume, kiitwacho Prostate Antigen (PSA). PSA huonesha kuwapo kwa tatizo kwenye Tezi Dume, lakini kipimo hiki hakina uwezo wa kutofautisha endapo tatizo hilo linamaanisha saratani.
Yafuatayo ni madhara ya tezi iliyotanuka:
- Kibofu cha mkojo kuuma: hivyo hupelekea mkojo kurudi juu, na kuharibu figo na Ini … … n.k.
- Kufunga kwa njia ya mkojo kabisa
- Figo kushindwa kufanya kazi (Kidney Failure)
- Kushindwa kumudu tendo la ndoa (Ndoa zinavunjika)
- Ugumba (Infertility, Frigidity for men)
- Kutokea kwa majipu sehemu ya Tezi Dume
- Kifo
Maoni
Chapisha Maoni