Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia wananchi wa Dodoma na Manyara baada ya kufungua barabara ya Dodoma-Babati ya KM 251 katika kijiji cha Bicha njiapanda ya Kondoa leo Aprili 27, 2018
Mchango wa +255 716 830 000: kuhusu Barbara hii anasema..
Sehemu ya barabara ya Dodoma-Babati ya KM 251 katika kijiji cha Bicha njiapanda ya Kondoa inavyoonekana leo Aprili 27, 2018 baada ya kufunguliwa na Rais Magufuli inapendezesha madhari ya eneo hill
Naye +255 769 487 676: ananauliza kuwa Viongozi wa kondoa chembe mumemsikia rais magufuli?
Kama majani yameota mpaka yakatoa maua njia nzima toka dodoma mjini hadi hapo alipofika ni kasoro ya viongozi wa wanaotokana na chama tawala.
Pia maji ya ntomoko viongozi hao hao wametafuna bilioni mbili. Anzeni kutafutana ili mrudishe hiyo pesa.
Mchango mwingine wa +255 769 487 676: anasema, Kama majani yanatoa maua, kwanini hajaona mazao kwa mfano wa hayo majani?
Naye +255 715 003 959: anasema Maswali kama hayo hutajibiwa sanasana utanuniwa tu.
viongozi wetu wanamadhaifu mengi sana lakini wamefanikiwa kwakiasi kikubwa kuwa nawapambe wanaowabigania kwahaliyoyote kuhakikisha wanawasafisha.
Tabia hii itutufanya tuwe naudumavu wamaendeleo endelevu.
Naye +255 769 487 676: anasema ndio maana hao viongozi tukiwauliza, utasikia nyinyi wapinzani ! Sasa rais kasema wasakwe hao pamoja na wapambe watupe pesa zetu mbilioni mbili za maji ya Ntomoko.
+255 715 003 959: Tena wakati mwingine utakuta mpambe anayehangaika kumsafisha kiongozi mbovu yeye mwenyewe na jamii yake wanataabika naukosefu wa huduma za afya elimu maji safi nk.
Ila kwasababu ya njaa na kukosa mbinu zakujikwamua ndo inabidi kujipendekeza na kuuza utu wako kwafaida ya soda na nauli za daladala.
Maoni
Chapisha Maoni