JPM atoa mifuko 300 ya saruji Arusha

Na Doreen Aloyce, Arusha

RAIS John Magufuli Ametekeleza ahadi yake kwa kutoa Mifuko 300 ya Saruji iliyokabidhiwa leo na katibu tawala mkoa  wa Arusha Richard Kwitega ,ikiwa ni siku moja tangu ameahidi itakayotumika kwa ajili ya ujenzi wa kanisa katoliki .

Rais Magufuli alitoa ahadi hiyo hapo jana April 8,mwaka huu katika Misa ya kuwekwa wakfu Askofu Isaac Amani  kuwa askofu mkuu wa kanisa hilo,iliyofanyika katika kanisa la mt,Thereza wa mtoto yesu ambapo Rais Magufuli alihudhulia.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo Kwitega amesema anajisikia faraja kukabidhi mchango wa Mh Rais Magufuli ambao umeweza kutimizwa kwa wakati kwa lengo la kutekeleza ujenzi wa kanisa hilo.

“Mhe Rais ameungana na waumini wa kanisa hilo katika kuchangia ujenzi huo na anajisikia amani kwa kushirikiana na waumini katika kuhakikisha kuwa kanisa hilo lina malizika mapema iwezekanavyo.

Kwa upande wake Paroko wa parokia  hilo Padri Paulo Malisa ambaye alikabidhiwa mchango huo amempongeza Rais Magufuli kwa hatua ya kutekeleza ahadi yake kwa muda mfupi na kuahidi kuendelea kumwombea ili aendelee kuwa na afya njema aendelee kuwahudumia watanzania wengine wenye uhitaji

‘’Tunamshukuru  sana s kwa Rais ahadi yake ikiwa ni siku moja tu tangu ameahidi tunaona ni jinsi gani rais wetu alivyokuwa wa vitendo zaidi kuliko maneno ,hata sisi tunashangaa zaidi kupokea leo hii tulitarajia labda ingechukua Mwezi ama Miezi’’amesema padre Malisa

Padri Malisa amesema kuwa malihiaji ya kanisa hilo bado ni makubwa kwani hadi sasa wanahitaji zaidi michangi kwani hadi kukamilika kwa kanisa hilo litagharimu kiasi cha shilingi bilioni 7

Naye paroko msaidizi wa parokia hiyo,Padri Festus Mangwangi amesema kuwa kanisa hilo limeanza kujengwa tangu mwaka 2011 na linajengwa kwa nguvu za wananchi  na hadi sasa kiasi cha shilingi bilioni 4 zimeshatumika .

Amesema kanisa hilo litakuwa na uwezo wakupokea waumini 3000 kwa mkupuo na litakuwa na sehemu tatu za kukaa waumini pia litakuwa na sehemu ya kuzika Maaskofu itakayokuwa chini ya kanisa hilo,{GROUND FLOW}

Hata hivyo amesema changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni wachangiaji  kutotekeleza kwa wakati michango  yao jambo ambalo linachangia kuchelewesha ujenzi wa kanisa hilo ambao kwa sasa umefikia katika hatua ya kuweka paa.

Maoni