KAMANDA WA POLISI MKOA WA DAR ATOA TAHADHARI

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa, mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya ya jiji la Dar es Salaam zimesababisha watu tisa kufariki dunia.

Wakati huo..

Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani kimeingiza sh bilioni 1.3 baada ya kukamata magari 35,115 yenye makosa mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Jana,Kamanda wa Kanda Maalumu,Lazaro Mambosasa amesema kuwa Fedha hizo zimetokana na tozo zilizochukua kwenye magari yaliyokua yanavunja sheria ya Usalama barabarani katika kipindi cha kuanzia Machi 30 hadi Aprili 12 mwaka huu.

Alisema katika kipindi hicho wameweza kukamata idadi ya magari 32,361,pikipiki 9006, daladala 12,321, Bodaboda wasiovaa kofia ngumu,60 na tayari wamefikishwa mahakamani, magari mengine makubwa yakiwamo malori 20 na gari ndogo  40 ambapo yamefanya jumla kuu kufikia 35,115.

Alisema jeshi hilo litaendelea kufanya kufanya ukaguzi wa Mara kwa Mara barabarani ili kuhakikisha madereva wanafuata sheria.

Maoni