ADHA YAWAKUMBUSHA KUJENGA ZAHANATI MPINJI
Kati ya vijiji vinne vilivyopo Kata Mpinji, ni Kijiji cha Kironge pekee hakina zahanati. Ambapo wananchi wanapata Huduma umbali wa km. 4 inayohusisha kuvuka mto Na kusababisha Adha Na madhara kwa wagonjwa.
🔹Wananchi wa Kijiji cha Kironge wa kishirikiana Na DC Same Na Halmashauri, wameamua kuanza Na kukamilisha ujenzi wa zahanati mwaka ujao wa fedha 2018/2019. Waanza kusafisha eneo la ujenzi kwa njia ya msaragambo.
🔹DC Asikiliza kero za wananchi hao Na kuzitolea ufafanuzi baada ya kazi.
🔹Yaelezwa Mpinji kuwa kata ya 3 kwa ukusanyaji mapato ikiongozwa Na Ruvu Na Ndungu.
🔹Wahimizwa kuzingatia ubora katika uuzaji wa Tangawizi, DC aahidi kuwaagiza wakala wa vipimo kuja kupima mizani.
🔹Serikali yaahidi kuhakikisha majengo ya kidato cha 5&6 yanakamilika, wananchi wapongezwa kwa juhudi ya ujenzi.
🔹Wapewa taarifa ya serikali kuleta umeme kijijini Hapo kwa mpango wa REA III.
Waelezwa mpango mpya wa iCHF wa kutibiwa hadi ngazi ya Mkoa.
DC atatua mgogoro wa Ardhi wa muda mrefu kati ya shule Na Mzee Kimbute.
" Same is not same"
Maoni
Chapisha Maoni