DC MBULU MGENI RASMI UCHANGIAJI DAMU SALAMA

Mkuu Wa Wilaya ya mbulu mh Chelestino  Mofuga Leo alikuwa mgeni rasmi katika uchangiaji wa damu salama wilayani Mbulu mkoani Manyara.

Akiongea na wananchi, wageni waalikwa, amepongeza jumuiya ya kanisa katoliki jimbo la mbulu kwa ushirikiano na serikali awamu ya tano kwani wanatoa huduma za kijamii

Baadhi ya huduma hizo ni Afya kwa kuchangia mashuka 70 kwa ajili ya wagonjwa wa chumba cha upasuaji katika hospitali ya Wilaya ya mbulu.

Makamu Askofu Jimbo katoliki la mbulu padre Orbanus sulle amewaomba wananchi kuchangia damu salama ili kuwasaidia watu wenye uhitaji wa damu.

Mkuu huyo wa Wilaya alisem, asilimia kubwa ya wananchi hapa nchini wanaopoteza maisha kwa kuishiwa na damu salama hasa wanawake na watoto.

Mgaga mfawidhi wa hospitali ya Wilaya ya mbulu Dr Magasi aliwataka wananchi kuacha hofu kwani kutolewa damu kuna mfumo maalum ndani ya mwili.

Alisema kuna kiwango cha damu kinachotakiwa kabla ya kutolewa damu kwaajili ya mgobjwa.

Mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza waendesha vyombo vya moto kama bodaboda na magari kuchangia damu salama ili kuongeza nguvu ya kuwasaidia wengine.

Hata hivyo vijana Wilayani Mbulu walishindwa kujitokeza katika vipaji vyao kama uimbaji hivyo kuishia kunywa pombe ambapo katika vipaji hiyo wanajitokeza hakina bibi na watoto (Damu ni uhai nipe niishi)

Maoni